WAANDAMANA KUDAI TAARIFA SAHIHI KIFO CHA MARADONA



WATU wa Argentina wameandama kudai taarifa sahihi ya kifo cha Diego Maradona.Waandamanaji hao ambao waliongozwa na aliyekuwa mke wa Maradona pamoja na mabinti wake wawili walidai kuwa kulikuwa na uzembe fulani uliopelekea kifo cha Mfalme huyo wa Soka.Wanataka ukweli uwekwe wazi.



Jumatatu bodi ya madaktari Argentina iliketi ili kuchunguza kuhusu taarifa sahihi ya kifo cha Maradona kama mahakama nchini humo ilivyoelekeza.Maradona mshindi wa kombe la dunia anaendelea kuheshimika Argentina kwa kipaji chake licha ya kuwahi kutumbukia kwenye madawa ya kulevya


0 Comments:

Post a Comment