BARAZA la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Same limepitisha bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kiasi cha bilioni 39.6 ili kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo wilayani hapo.
Anastazia Tutuba ni katibu wa baraza hilo ambaye pia ni mkurugenzi wa halmshauri aliisoma bajeti hiyo katika kikao maalum cha baraza la madiwani na kusema kuwa vipaumbele katika bajeti hiyo ni pamoja na kutenga mafungu maalumu kwa ajili ya utoaji elimu ya ukusanyaji mapato
Alisema bajeti hiyo imetenga fungu la kuboresha Miundombinu ya umwagiliaji, elimu ya lishe , pamoja kutenga fungu kwa ajili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu vivutio vya Utalii vilivyopo wilayani humo.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo ni wataendelea kujikita katika nyanja mabalimbali za utoaji huduma kwa jamii kama vile, elimu, miundombinu ya barabara, afya, maji, na umeme na huduma nyinginezo za kijamii.
Alisema katika kufikia malengo ya ukusanyaji huo wa mapato halmashauri hiyo imebuni vyanzo vipya vya ukusanyaji wa mapato,na kwamba wataanza kukusanya ushuru wa magari yanayobeba madini ya jipsam na kupeleka nchi za nje na ndani ya nchi .
"Katika kata ya Makanya pale kuna mapori yanayokuja kuchukua madini ya jipsum hivyo kwa sasa tunaanza kuchukua ushuru"alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Yusto Mapande, alisema asilimia kubwa ya bajeti inaenda kulipa mishahara ambazo ni zaidi ya sh28.3 bilioni ambapo zitalipa watumishi 4,803.
Alisema katika bajeti ya sh39.6 bilion zaidi ya sh 2.5 bilioni zinatokana na vyanzo mbalimbali vya makusanyo ya mapato ya ndani.
Na Gift Mongi, Same.

0 Comments:
Post a Comment