WATENDAJI SERIKALINI SIKILIZENI KERO ZA WANANCHI



 

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka viongozi na watendaji wote wa Serikali wahakikishe wanawafikia wananchi kwenye maeneo yao, kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi badala ya kusubiri ziara za viongozi wakuu wa Kitaifa

 

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Februari 5, 2021) wakati akihitimisha hoja ya kujadili hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa bunge la 12 Novemba 13, 2020. Amesema watendaji hao wana wajibu kwa wananchi kutokana na dhamana waliyowapatia.

 

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa kila mtendaji Serikalini ahakikishe anatimiza wajibu wake kikamilifu na wale wote watakaokiuka sheria, kanuni na taratibu za kazi watachukuliwa hatua na kamwe haitomvumilia mtumishi mzembe na mwenye kufanya kazi kwa mazoea.


Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wabunge kwamba maoni na hoja zao zitazingatiwa wakati wote wa utekelezaji wa vipaumbele vya Serikali.

 

Amesema kuhusu miradi inayoendelea kutekelezwa nchini katika sekta za uzalishaji mali ikiwemo kilimo, mifugo, maliasili, madini na sekta za huduma ya jamii, kama vile elimu na afya nayo itakamilishwa kama ilivyokusudiwa.

0 Comments:

Post a Comment