MWILI WA BALOZI KIJAZI ULIVYOPOKELEWA DAR





Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo, Februari 18, 2021 ameongoza mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.





Viongozi wengine walioshiriki katika Mapokezi hayo ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndubaro na Katibu Mkuu  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas.
☝🏽Habari katika picha


Mwili wa marehemu Balozi Kijazi utaagwa kesho Ijumaa Februari 19, 2021 katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam na kisha kusafirishwa kwenda Wilayani Korogwe, Tanga kwa ajili ya mazishi.


0 Comments:

Post a Comment