Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA, John Mnyika ameongoza mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa chama hicho, Arcado Ntagazwa nyumbani kwake Kimara jijini Dar es Salaam.
Ntagazwa alifariki dunia Jumatano Februari 10, 2021 katika hospitali ya Mloganzila alikokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa jumamosi Februari 13, 2021 jijini Dar es salaam.
Akitoa salamu kwa niaba ya chama hicho, Mnyika amesema siku chache kabla ya kufikwa na mauti, Ntagazwa aliwaagaa kwa sala baada ya kuhitimisha vikao vya Chadema vilivyokuwa vikifanyika Zanzibar.
"Alikuwa ni mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa chama na mjumbe wa kamati kuu, siku chache kabla ya umauti alituaga kwa sala baada ya kuachana kwenye vikao vya chama. Yeye ametangulia sisi tutaendelea kuheshimu michango yake lakini pia tutaendelea kusimamia yale aliyoyaamini," amesema Mnyika.
WASIFU WA NTAGAZWA
Akisoma wasifu wa baba yake, Thomas Ntagazwa amesema enzi za uhai wake alishika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo ya naibu waziri wa fedha, ujenzi na ardhi na aliwahi kuwa mbunge wa Muhambwe kwa miaka 25. Ntagazwa alihamia Chadema mwaka 2010 akitoka CCM.

0 Comments:
Post a Comment