MACHINGA WAJIKATIA MAENEO STENDI MPYA YA MAGUFULI

 

Wafanyabiashara hao wameanza kujikatia maeneo katika eneo la nje ya Kituo cha mabasi ya mikoani cha Magufuli  kwa ajili ya kufanya biashara, pia baadhi ya waendesha pikipiki wameanza kujisajili kuwa waendesha pikipiki wanaotambulika katika Kituo hicho.


Hatua hiyo imetokana na agizo la Rais John Magufuli  kwa Waziri wa TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo kuhakikisha kutobuguziwa kwa Wafanyabiashara wadogo wadogo (Machinga) katika Kituo Kikuu cha Mabasi Magufuli Jijini Dar es Salaam.


Rais, John Magufuli alipokuwa akikata utepe kuashiria Uzinduzi Rasmi wa Kituo Kikuu cha Mabasi kilichopo Mbezi jijini Dar es salaam, kituo ambacho kitatumika na Wananchi, Mabasi yaendayo nje ya nchi  na na yale yaendayo mikoani


0 Comments:

Post a Comment