MACHIFU WAOMBA KUMPATIA TUZO JPM


UMOJA wa machifu nchini(UMT)umeahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kutunza kumbu kumbu mbalimbali  za kihistoria  ambazo zimeonekana kusahaulika kwa kurithisha vizazi vya sasa kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo.



Mwenyekiti wa umoja huo, Chifu Frank Marialle alitoa tamko la umoja huo katika hafla ya kumpongeza rais Dkt John Magufuli kwa kutambua umuhimu wake machifu Mara baada ya kuzindua soko la Morogoro ambalo alitaka liitwe jina la Chifu Kingalu.


Alisema kutokana na kitendo hicho ni dhahiri serikali ya awamu ya tano in Nia madhubuti ya kutambua umuhimu wa machifu nchini kwa kuweka historia mbali mbali ambazo zilianza kufutika na kuwa kwa Sasa zinaanza kuenziwa kwa maslahi ya vizazi vilivyopo.


"Tunamshukuru Sana Rais, (Magufuli) kwa kuona umuhimu wa kutunza kumbu kumbu za machifu hapa nchini na hata juzi alizindua soko pale Morogoro akataka liitwe Kingalu ambaye alikuwa ni Chifu wa pale na sisi tumejipanga kuhakikisha tunashirikiana na serikali katika kuwezesha kumbukumbu hizi kihifadhiwa"alisema chifu Marealle.


Kwa mujibu wa Marialle ambaye pia ni Chifu/Mangi wa Marangu ni kuwa serikali imedhamiria historia za machifu  ziwekwe kwenye mitaala tayari kwa kufundishishwa shuleni na kuwa tayari wameshaandaa historia hiyo na kuikabidhi serikalini kupitia taasisi ya elimu nchini TEA .


Chifu Marialle pia ameendelea kumuomba Rais Dkt Magufuli kukubali ombi la machifu hao kumpatia tuzo maalum kwa kutambua umuhimu wa machifu katika jamii za kitanzania sambamba na uongozi wake uliotukuka katika kulivusha taifa katika mambo mbali mbali


"Tunaendelea kumuomba akubali ombi letu la tangu mwaka jana tulikompelekea tunatambua mchango wake mkubwa katika taifa letu na alipotuvusha lakini pia ana mchango kwa kutambua umoja wetu huu"alisema


Hata hivyo umoja huo ulikadhi nakala za miongozo serikali za namna machifu walivyokuwa wanaongoza sambamba na namna wakivyoshiriki kwenda umoja wa mataifa kuomba uhuru wa Tanganyika ili iwe kumbukumbu kwa watu wanaotaka kufuatilia historia za machifu na kazi zao hapa nchini


Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya Elimu  Tanzania, (TEA) Aneth Komba ,alisema wamekutana na umoja wa Machifu nchini (UMT)ili kupata historia ya nchi,  namna walivyoshiriki katika upatikanaji wa Uhuru ili kuweza kuweka kumbukumbu sawa kwa vizazi vilivyopo na vijavyo na kuepuka upotoshwaji.

Alisema lengo la kukutana na machifu hao ni kupata historia ya nchi ambayo iko akilini mwa machifu na haijawahi kuandikwa popote ili iweze kuwa rahisi kuwekwa katika mitaala ya kielimu ya vizazi vijavyo waweze kuipata.

Alisema lengo muhususi ni kuiweka katika mitaala ya elimu ambapo itafundishwa shuleni kuanzia elimu ya awali have kidato cha sita ili kuweka uelewa sawa tofauti na ilivyo sasa.

 Na Gift Mongi, Moshi.


0 Comments:

Post a Comment