WAAFRIKA TUANDAE MAUDHUI YETU MITANDAO - TAMASHA LA KAN

 

WAAFRIKA wanatakiwa kuamka na kuandika maudhui yanayowahusu kwenye mitandao na vyombo vya habari jambo litakalosaidia kuonyesha uhalisia wa yale yanayoendelea tofauti na sasa ambapo maudhui yanaelezea mambo hasi zaidi.



Akiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mshiriki wa tamasha la KAN Festival Carol Ndosi, alielezea mjadala uliovuta hisia za wengi  kuhusu maudhui ya bara la Afrika namna yalivyo na nani ana wajibu wa kuyaweka katika majukwaa ya kidigitali na kwenye vyombo vingine vya habari.


"Nani anajukumu la kutuongelea sisi kama Waafrika, kwaaba waafrika tunafanya nini, maendeleo yetu sisi yakoje, changamoto tunazopitia na mpaka sasa hivi yumepiga hatua gani kimaendeleo," anasema Ndosi na kuongeza.

... Kwa sababu kinachoonekana kwa sasa maudhui mengi yaliyopo kuhusu bara la Afrika ni hasi. Yanaonyesha upande mmoja tu na bahati mbaya sana maudhui mengi hayaendeshwi na sisi wewe wenyewe,".

...Tulikuwa tunaangalia ni jinsi gani wabunifu na jamii kwa ujumla namna gani tunaweza kubadilisha maudhui yetu yaliyo mtandaoni na majukwaa mbalimbali yalenge kusukuma maendeleo ya bara letu la Afrika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tamasha la Kan Festival  Khalifa Mbowe alisema kuwa tamasha la Kan linawasaidia wananchi kujisikia kuwa wao ni sehemu ya maendeleo ya nchi zao kwa kujiona wao ni fursa ya ndiyo majawabu ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya Afrika.

Tamasha hilo limewakutanisha  wasanii mbalimbali wa muziki kutoka nchi za Afrika Mashariki akiwemo G nako, Nikki wa pili Nazizi Grece Matata, Tarajazz Richie, Worriors from the East na Dj Skadi ambapo limeanza January 28 na kuhitimishwa Januari 30 huku asilimia 85 ya tamasha hilo likifanyika mtandaoni kutokana na changamoto ya Corona inayoendelea kuikabili dunia hivi sasa.

Tamasha hilo linalofanyika katika viwanja vya chuo cha Maendeleo na uhusiano wa kimataifa (Ms-TCDC) kilichopo ndani ya Wilaya ya Arumeru.

0 Comments:

Post a Comment