MATRILIONI YA FEDHA YATUMIKA MITANDAONI KWA MWEZI0

SERIKALI inapata kiasi cha sh. Bilioni 80 kwa mwezi kama tozo kutokana na Tsh. Trilioni 18 zinapita kwenye mitandao kwa mwezi.



Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile ameiarifu Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu.


Amesema miamala inayofanyika na tozo ambazo Serikali inapata ni kutokana na kuwepo kwa matumizi ya TEHAMA ambapo jumla ya miamala Milioni 300 inafanyika kwa mwezi mtandaoni na Serikali.


Dkt. Ndugulile amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa,  Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ni njia kuu ya uchumi na inawezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano yenye kasi, kufanikisha utendaji kazi wa mifumo ya TEHAMA na huduma za fedha mtandaoni.

Amesema  Wizara imejipanga kuandaa ramani ya njia ya miundombinu huo ili kufanikisha mwingiliano wa ujenzi na upanuzi wake pale inapokutana na njia za miundombinu mingine kama vile ya barabara, maji, umeme na reli.

Kikao hicho pia kilichohudhuriwa na wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo na wakuu wa taasisi zake, Dodoma.

0 Comments:

Post a Comment