MAREKANI YAWAONDOLEA VIKWAZO RAIA WA TANZANIA

 Rais mpya wa Marekani, Joe Biden amewaondolea raia wa Tanzania vikwazo vya kushiriki bahati nasibu ya viza, ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya kutangazwa kwa vikwazo hivyo.



Januari 30, 2020 serikali ya, Donald Trump ilitangaza kuwawekea Watanzania vikwazo vya kushiriki bahati nasibu hiyo pamoja na raia wa nchi nyingine kadhaa.

Jana Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulitangaza kuwa marufuku hiyo imefutwa rasmi na rais mpya wa nchi hiyo, Joe Biden aliyeingia madarakani jumatano wiki hii.


"Mojawapo kati ya hatua zake za mwanzo kabisa akiwa Rais, Rais Biden ameondoa kikwazo kilichowekwa kwa Watanzania kuomba Viza ya Bahati Nasibu (Diversity VISA - DV)," ubalozi huo umeandika kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Januari 30, 2020 serikali ya Donald Trump ilitangaza kuwawekea Watanzania vikwazo vya kushiriki bahati nasibu hiyo pamoja na raia wa nchi nyingine kadhaa.

"Nchi hizi, kwa sehemu kubwa, zinataka kutoa msaada lakini kwa sababu mbali mbali zimefeli kufikia viwango vya chini tulivyoviweka," aliyekuwa Naibu Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Chad Wolf aliwaambia wanahabari baada ya kutangazwa kwa vikwazo.

IFAHAMU VIZA YA BAHATI NASIBU HIYO







Bahati nasibu hiyo ilipitishwa kisheria nchini Marekani mwaka 1990 na bahati nasibu ya kwanza ikafanyika mwaka 1995.

Toka wakati huo, takribani watu 50,000 kila mwaka kutoka nchi mbalimbali duniani hushinda bahati nasibu hiyo na kupata viza ya kuingia Marekani na kufanya kazi kama wakazi wa kudumu.

Washindi wa viza hiyo pia huweza kuhamia nchini humo na wenza wao pamoja na watoto walio chini ya umri wa miaka 21.

Kwa mujibu wa taarifa za Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, katika kipindi cha miaka 10 kuanzia kwama 2008 mpaka 2018 jumla ya Watanzania 643 walishinda bahati nasibu hiyo.

Katika kipindi hicho, mwaka ambao Watanzania walishinda wengi zaidi ilikuwa 2009 watu 137 na mwaka ambao walishinda wachache ilikuwa mwaka 2014 watu 28.

Zaidi ya Watanzania 10,000 hutuma maombi ya kushiriki bahati nasibu hiyo.

Hata hivyo, ushiriki na ushindi wa Watanzania ni mdogo ukilinganisha na baadhi ya mataifa barani Afrika.

Sudan nayo ambayo imepigwa marufuku kama Tanzania katika kipindi hicho cha mwaka 2008-2017 raia wake 8,127 walishinda bahati nasibu hiyo.

Majirani wa Tanzania nchi ya Kenya katika miaka 10 hiyo imeshuhudia raia wake 15,172 wakishinda bahati nasibu hiyo.

Kwa mwaka 2017 pekee, Wakenya 360,023 walituma maombi, kati yao 249,397 waliingia kwenye kinyang'anyiro na mwishowe walioshinda bahati nasibu walikuwa 1,014.


Kwa hisani ya BBC

0 Comments:

Post a Comment