MAJALIWA AONGEA MAZITO MSIBA WA MBUNGE VITIMAALUM

 WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia (CCM) mkoa wa Manyara Martha Umbulla na ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi wamuezi kwa kuyaendeleza mambo mema aliyoyafanya katika kipindi cha uhai wake.

 

 


Mazishi hayo ya Martha yamefanyika jana  nyumbani kwake katika kijiji cha Dongobesh wilayani Mbulu mkoa wa Manyara.

“Nimekuja kuungana nanyi kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kutoa pole kwa mume wa marehemu, watoto na familia kufuatia msiba mzito wa kuondokewa na mpendwa wetu Mheshimiwa Umbulla.”


0 Comments:

Post a Comment