Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Salum Hamduni
Mkazi wa Sakina, Olaiis Wavii (46) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu.
Inadaiwa mtoto huyo anayesoma shule ya awali ya New Life alibainika kuwa na tatizo la kutokwa na haja ndogo mfululizo ndipo ikabidi afanyiwe uchunguzi wa kitababu ikabainikwa kuwa anabakwa.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha, (RPC), Salum Hamduni ametoa taarifa kwa vyombo vya habari jana na kueleza kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi.
Alisema kuwa tukio hilo lilijulikana januari 25, mwaka huu majira ya saa 4:30 asubuhi
kwenye katika kijiji cha Olosiva, kata ya Olorieni wilayani Arumeru.
Kamanda Hamduni alisema kuwa alibaini tukio hilo nk afisa ustawi wa jamii wa eneo hilo, (hakumtaja jina) wakati akiwa anaendelea na shughuli
zake maeneo ya kijiji hapo.
" Afisa ustawi wa jamii alibaini kuwa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu jina limehifadhiwa mwanafunzi wa shule ya awali iitwayo NEW LIFE iliyopo Olasiva Sakina akiwa anatokwa na mkojo mfululizo," alisema Kamanda Hamduni na kuongeza.
...Ndipo alipotoa taarifa katika kituo cha polisi na baadaye kufanya uchunguzi wa kitabibu ndipo alipo gundulika kuwa mtoto huyo amebakwa,".
...Jeshi la polisi Mkoani hapa lilianza uchunguzi wa tukio hilo na kubaini baba mzazi aitwaye OLAIIS S/O WAVII (46) mmasai na mkazi wa sakina ndiye aliyembaka mtoto huyo,".
RPC, Hamduni, alisema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi na mara baada ya upelelezi kukamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa ajili ya hatua.
"Natoa wito kwa wazazi na walezi wenye tabia ya kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kuacha vitendo hivyo mara moja kwani ni kinyume na taratibu za nchi," alisema Kamanda Hamduni na kuongeza.
....Pia niyaombe madhebu ya dini kuwakumbusha na kuwapa elimu waumini wao kwenye nyumba za ibada,".

0 Comments:
Post a Comment