Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema serikali imesitisha makongamano na mikutano ya mkesha wa mwaka mpya katika maeneo yote ya wazi kutokana na sababu za kiusalama.
Ametoa tamko hilo jana jijini Dodoma ambapo amesema makongamano na mikutano hiyo ifanyike kwenye maeneo ya nyumba za ibada na mwisho iwe ni saa sita na nusu usiku.
Aidha katika hatua nyingine Simbachawene amempongeza askari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji wilayani Ngara mkoani Kagera kwa kitendo cha kishujaa cha kumuokoa mtoto aliyetupwa chooni.

0 Comments:
Post a Comment