Jade Simmons ni mpiga piano na mshauri nasaha, mzaliwa wa Marekani na fundi wa mitambo mawasiliano ya kiteknolojia na bilionea wa sarafu ya dijitali - wanasimamia nini, na kwanini wanastahili kura za Wamarekani.
Malikia huyo wa zamani wa urembo pia ni mpiga piano wa tamasha la kitaalam, mshauri nasaha, rapa, mama, na mchungaji aliyeteuliwa.
Kama anavyosema, yeye ni mgombea binafsi asiyekuwa wa kawaida, "lakini kuna nyakati ambazo sio za kawaida ".
"Kwangu mimi huu ni wakati ambao hatuwezi kufanya mambo kama kawaidal," anasema "Mimi ni binti wa mwanaharakati wa kupigania haki katika jamii, pia naomba mjue kuwa baba yangu alinifunza kutonyamaza nisiporidhika na mambo yalivyo, ukiona haki inakiukwa unahitaji kujiuliza laiti ni mimi ningelifanyaje."
Anasemalengo lake ni kubuni nafasi sawa kupitia uchumi, elimu na mageuzi ya mfumo wa haki. Na kutokana na malengo hayo "anapania kuendesha kampeni isiyo na gharama katika historia ya nchi yetu".
MRENGO WAKE
"Inategemea swali hilo umemuuliza nani!" anasema. "Kila kitu kutoka kwa wanaolalamika kinyonge hadi wahafidhina makanisani wanapenda sera zetu."
Anasema malezi yake ya kihafidhina na mpenda dini hayajamfanya yeye kuwa mhafidhina moja kwa moja , anasema.
Janga la corona limevuruga kwa kiwango kikubwa kinyang'anyiro ch akuingia Ikulu ya White kwa kuzuia mikusanyiko ya watu, hali iliyolazimu vyama vya kisiasa kunadi sera katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Lakini kwa Jade, changamoto kubwa iliyokumba kampeni yake ni kujitambulisha kwa watu wajue naye yuko katika kinyang'anyiro hiki.
"Hata wakati wa ambapo ulimwengu uliangazia suala la maisha ya watu weusi yana umuhimu watu walikuja pamoja kuzungumzia suala hilo kupitia vyombo vya habari na mashirika ya kijamii - lakini vyombo hivyo vya habari vilikataa kusema niko hapa.
"Huenda umemsikia msanii maarufu kama Kanye West ambaye hata hakuwasilisha makaratasi yake lakini Julai tarehe nne alipotangaza kuwa tagombea urais ndani ya dakika 30 taarifa yake iliangaziwa katika vyombo vyote vikuu vya habari. Kwa hivyo tulishangaa sana kuona suala la demokrasia halipo kama wanavyodhania wapiga kura wa Marekani hasa ukilichunguza kwa undani."
Wakati wagombea walioteuliwa na Republican na Democratic watakuw akatika karatasi ya kupiga kura katika majimbo yote, wagombea binafsi lazima wafikia masharti kadhaa kabla ya kupewa idhini ya kugombea.
Jina la Bi Simmons lilichapishwa katika makaratasi ya kupiga kura katika majimbo ya Oklahoma na Louisiana, lakini katika majimbo mengine 31 alisajiliwa kama mgombea atakaye andikwa jina - kumaanisha ikiwa wapiga kura wataandika jina lake katika karatasi ya kupiga kura basi kura yake itahesabiwa. Anakubali kuwa hali ilivyo hana uwezo wa kufikia ndoto yake kwa sasa, lakini anaamini siku moja ataingia ikulu.
Marekani imekuwa na marais kwa zaidi ya miaka 230, lakini - George Washington - ndiye wa kwanza kuchaguliwa kama mgombea binafsi.
Siasa za vyama vya Republican na Democratic zimeangaziwa zaidi na vyombo vya habari kiasi cha kuwa ni vigumu mtu yeyote kutoka nje ya vyama hivyo kushinda uchaguzi.
Kufikia Octoba 9, wagombea 1,216 wa urais waliwasilisha maombi ya kutaka kuwania kiti cha urais wa Marekani kwa Tume ya Uchaguzi.
Source BBC

0 Comments:
Post a Comment