Kamala Haris, aliyepeleka jela watu 1500 kwa uuzaji na matumizi ya bangi. Wakati wa kampeni aliahidi kurekebisha sheria na kuhalalisha mmea huo.
Mwanasheria mzuri kuliko wote nchini Marekani (nimeongeza chumvi kidogo tu) ila hayo ni maneno ya Aliyekua rais wa Marekani, Barack Obama kwenye sherehe ya uchangishaji fedha kupitia chama chake cha Democratic huko kwenye kitongoji cha SanFrancisco mjini Califonia ambapo Kamala alikua ndiye manasheria mkuu mjini humo.
Obama alisema.
"Lazima uwe mwangalifu, kwanza huyu bi dada ni mkali, yupo imara na pia ndiye mtu tunayemuhitaji katika kusimamia masuala ya sheria, pia kwa mbaaali ukimwangalia anaonekana ndiye mwanasheria mkuu mwenye muonekano mzuri nchini humu.
Kauli ilizua utata na wengine waliikanyaga kwa kusema amemdhalilisha japo wao ni watani kama George Bush na mke wa Obama.
Kamala Harris, amezaliwa Califonia Marekani mnamo Oktoba 20 mwaka 1964. Mwanamama ambaye ulimwengu wa siasa ulimtambua pale mwaka 2016 alipochaguliwa kama Seneta kupitia chama chake cha Democratic na kuiwakilisha vyema Califonia. Hapo kabla alikua ni mwanasheria wa serikali kwa mwaka 2011 hadi 2017.
Hajaanza kuvunja rekodi leo - bali hata alipokuwa Seneta alikuwa ndiye mwanamke wa kwanza mmarekani, mwenye asili ya uhindi (ASIA) kutumikia useneta nchini humo na pia mwanamke wa pili mwenye asili ya uafrika (Mweusi).
Je Unashangaa?
Usishangae, mama huyu ana asili ya Afrika na India. Baba yake ni Donald Harris mhamiaji kutoka nchini Jamaica ambaye kitaaluma ni mchumi huku mama yake Shyamala Gopalana akiwa na mhindi tena mtaalamu wa uchunguzi kuhusu magonjwa ya kansa, unaambiwa upande wa mama yake mababu na mabibi ni Matabibu wazuri sana.
Pia Jina lake la Kamala ni la kihindi likimaanisha nguvu kubwa, kwa waumini wa kihindu hili pia ni jina lingine la mungu wa kike *LAKSHIMI* aaah msinirudishe kwetu kwa wazee wa kuchkuch. Ninaye kusimulia hapa ni mimi Humphrey Moris na wala sio Juma KhanSmiling face with open mouth and tightly-closed eyes.
Baada ya wazazi kupeana talaka, Kamala na dada yake Maya walilelewa na mama yao huku wakihudhuria sala za wahindu na kanisa la Baptist. Huku akiwa hasiti kumtaja mama yake kama mwanamke jasiri na role model wake number 1
Alikwenda high school huko Canada wakati mama yake akiwa anafundisha chuo kikuu cha McGill. Baadae alirudi Mjini washington kusoma sayansi ya siasa na uchumi huko Howard University chuo chenye historia tam ya watu weusi. Na baadae alirudi Califonia kwaajili ya masomo ya sheria.
Akabahatika kufanya kazi kwenye ofisi ya mwendesha mashitaka wa Alameda huko kwenye kitongoji cha Oakland, ambapo kazi yake kubwa ilikua kufuatilia kesi za masuala ya jinsia.
Akawa mshindi kwenye ofisi ya wakili wa wilaya huko San Franscisco mwaka 2003 na kuwa juu ya boss wake wa zamani na kuvunja rekodi nyingine kwa kuwa mwanamke wa kwanza mweusi mjini Califonia kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo (kama huwezi kusema Amin, basi we ni mchawi- I rebuke you)
Wakati huo alikua na mahusiano na mwanasiasa fulani huko Califonia (Willie Brown) ambaye alimzidi Kamal miaka 30 (babu aliopoa ngoma bwana, dj naomba unipigie nyimbo ya king kiki kitoto chaanza tambaa) Lakini waliachana pale jamaa alipochaguliwa kuwa meya wa san francisco
Mwaka 2010 aliingia kwenye kinyang'anyiro cha nguvu kuwania nafasi ya uwanasheria mkuu dhidi ya mwanasiasa maarufu na Mwanasheria wa wilaya mstaafu wa mjini Los Angeles bwana steve cooley, na alishinda.
Mwaka 2012 aling'ara sana kwenye chama hasa kwenye suala la kujitoa na baadae aliolewa tena na Douglad Emhoff. Akapikwa kwaajili ya kuchukua kiti cha seneta Barbara Boxer ambaye alikua anastaafu. Na katika kampenzi zake alizungumzia suala la kubadili sheria za wahamiaji na makosa madogo madogo suala ambalo lilimpatia kiti kiulaiiiiini mwaka 2016.
Ikumbukwe Alipokaa kwenye kiti mwezi wa kwanza mwaka 2017 akawa anafanya kazi mbili (siasa na sheria) unaambiwa alikua wamoto sana kwenye kuhoji, tena kwa mtindi wa kukuuliza swali na kukuacha ujimwage na hapo anakukosoa. Kumbuka alitikisa ndevu za wazee kwa maswali magumu kwa mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwa malalamiko ya Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Alitia nia ya urais wa mwaka 2020 na akaingia kwenye majibizano makubwa na Joe Biden kwenye kugombania hiko kiti. Kamala alipinga sera ya Biden ya kusimamisha school bus kwa kujitolea mfano yeye kama mwanafunzi ambaye alipanda school bus na zilimsaidia sana akiwa mwanafunzi. Lakini hadi kufikia mwezi wa 12 mwaka huo, alishindwa kuendelea na kampeni na kurudi nyuma.
Juhudi zake kwa kuomba mabadiliko kwenye sheria zilifunga midomo ya watu wengi na kumpatia wafuasi wa kutosha baada ya kifo cha George Floyd (mmarekani mweusi aliyefariki akiwa chini ya ulinzi, alifariki baada ya askari kutumia nguvu kubwa kumuweka chini ya ulinzi).
Kutokana na ubaguzi mkubwa nchini Marekani, wafuasi wengi wa biden waliomba awe na makamu shupavu na mtu wa rangi tofauti. Na mwezi wa nane mwaka 2020 Biden akamchagua mpinzani wake ndani ya chama, bi Kamala Harris ambaye kwa sasa ndiye makam wa rais wa kwanza mwakamke (mwenye asili ya Afrika na Asia)
Baada ya kuchaguliwa kuwania kiti na Biden, watu walisema mumetuchagulia mwanajeshi ili atunyooshe. Kumbuka miaka mitatu ya useneta jimboni kwake, alifikisha watu wengi makakamani kiwango cha hatia cha jiji kiliruka kutoka 52% hadi 67%. Harris pia alisimamia maamuzi kadhaa ya kutatanisha,ikiwa ni pamoja na kukataa kufuata adhabu ya kifo dhidi ya mtu aliyemuua afisa wa polisi Isaac Espinoza, swala lililosababisha umoja wa polisi kumtenga kwa muongo mmoja.
Bi dada Tulsi Gabbard
Akiwakilisha Hawaii alimshtaki Harris kwa kusweka ndani zaidi ya watu 1,500 jela kwa makosa yanayohusu uuzaji na matumizi ya bangi Nakumbuka Bi dada Tulsi alipoulizwa kwanini anawatetea wavuta bangi, au na yeye ni mtumiaji (ALIISHIA KUCHEKA). Ilisaidia kwasababu Harris aliitetea rekodi yake na kuahidi mageuzi ya kitaifa, pamoja na kuhalalisha bangi wakati wa kampeni za urais.
Imeandaliwa na @humphreymoris

0 Comments:
Post a Comment