Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage (kulia) jana Oktoba 23, 2020 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti na Kiongozi wa misheni ya watazamaji wa uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika mashariki, (EAC) ,Sylvestre Ntibantunganya ambaye pia ni Rais mstaafu wa Burundi.
Mazungumzo hayo yalijikita kuangazia juu ya mambo kadhaa yanayohusiana na Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Oktoba 28, 2020. Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam
kilihudhuriwa pia na Makamu wa Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu, Mbarouk Salim Mbarouk.


0 Comments:
Post a Comment