Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Karatu, Waziri Mourice, alimtangaza Daniel Awack, (CCM) kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupata kura 49,042 akifuatiwa na Cecilia Pareso, (CHADEMA), alipata kura 31,150 na Patrick Kaimu , (CHAUMA), aliambulia kura 424.
Msimamizi uchaguzi jimbo la Arumeru Magharibi, Saad Mtambule alimtangaza Noah Lebris (CCM) kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupata kura 72,160 akifuatiwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Gipson Ole Meseyeki, (CHADEMA) aliyepata kura 22,744, akifuatiwa John Kivuyo, (ACT Wazalendo) aliyepata kura 2,492.
Alitangaza wagombea wengine Mohamed Muya , (CUF) alipata kura 329, Loilole Wilson, (NCCR Mageuzi) 323 na Andrew Akyoo, (UPDP) 169.
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Arumeru Mashariki, Emmanuel Mkongo alimtangaza Dkt John Pallangyo ,(CCM) kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupata kura 84,858 akifuatia na Rebeca Mngodo,(CHADEMA) aliyepata kura 14,688.
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Arusha Mjini, Dkt John Pima alimtangaza Mrisho Gambo, (CCM) kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupata kura 82,480 huku mbunge aliyemaliza muda wake Godbless Lema, (CHADEMA) akipata kura 46,489, Thomas Kundi (AAFP) aliyepata,(831).
Wengine ni Mwinyi Hamis (ADA-TADEA ) aliyepata kura 249, Polycarp Shayo, (ACT Wazalendo), aliyepata kura 384, Godfrey Sembuche, (DP) aliyepata kura 33, Magdalena Shangai, (CUF) aliyepata kura (177) , Johnson Bayo (SAU) aliyepata kura 88, Elias Sumari, (UPDP) aliyepata kura 80, Nicolaus Molled, (UDP) aliyepata kura 66, Michael Mjema, (Demokrasia Makini), aliyepata kura 57, Reward Kiwelu, (NCCR Mageuzi) aliyepata kura 77, Rashid Jaralia, (NRA)
aliyepata kura 57, na Richard Membi, (CCK) aliyepata kura
243.
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Ngorongoro, Raphael Siumbu alimtangaza William Ole Nasha kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupata kura 63,536 akifuatiwa na Jackline Swai,(CHADEMA) aliyepata kura 7,783 na Supeet Ole Purko (ACT Wazalendo) aliyepata kura 831.
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Monduli, Stevin Ulaya alimtangaza Fredrick Lowassa,(CCM) kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupata kura 72,502 huku mshindani wake Cecilia Ndosi (CHADEMA) akipata kura 4,637 .
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Longido, Dkt Jumaa Mhina, alimtangaza Dkt Steven Kiruswa kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupata kura 61,885 akifuatiwa na Pauline Laizer ,(CHADEMA) aliyepata kura 1,037, Kombo Mutadam, (CUF) aliyepata kura 65 na Juma Feruzi, (NRA) aliyepata kura 21.
0 Comments:
Post a Comment