Manchester United kwa mara nyingine
wametangazwa kuwa klabu yenye thamani ya juu zaidi Ulaya, ambapo thamani
yao inakadiriwa kuwa €3.25bn (£2.9bn) kwa mujibu wa kampuni ya KPMG.
Klabu hiyo ya England inaongoza kwa "thamani ya biashara", ikiwa mbele ya klabu nyingine kama vile Real Madrid na Barcelona.
Orodha
hiyo imeandaliwa baada ya utafiti uliofanywa kwa kuangazia taarifa za
kifedha za misimu ya 2015-16 na 2016-17 ambapo waliangazia faida, haki
za utangazaji, umaarufu, matarajio kutokana na uwezo wa kimichezo na
thamani ya uwanja.
Liverpool, ambao wamefika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wamo nafasi ya nane kwenye orodha hiyo.
Kwenye utafiti huo ulioangazia klabu 32 kubwa, klabu za Ligi Kuu ya England zinajaza nafasi sita kati ya 10 za kwanza.
Andrea
Sartori, mkuu wa michezo duniani katika KPMG ambaye ndiye mwandishi wa
ripoti hiyo, anasema kwa jumla thamani ya klabu za soka imepanda katika
mwaka uliopita.
"Ukuaji wa jumla unatokana na sababu kadha, moja ikiwa ni
kuongezeka kwa mapato yanayotokana na uendeshaji shughuli katika klabu
32 kuu, ambao ulikuwa ni ukuaji 8%," alisema.
"Uhamisho wa
wachezaji wa pesa nyingi pamoja na kuongezeka kwa mishahara hakujazuia
klabu kuendelea kuongeza mapato, kwani faida kabla ya kutozwa ushuru
uliongezeka kwa mara 17 ukilinganisha na mwaka uliotangulia." Klabu 10 bora Ulaya kwa 'thamani ya biashara'
Manchester United - €3.255bn
Real Madrid - €2.92bn
Barcelona - €2.78bn
Bayern Munich - €2.55bn
Manchester City - €2.16bn
Arsenal - €2.10bn
Chelsea - €1.76bn
Liverpool - €1.58bn
Juventus - €1.30bn
Tottenham - €1.29bn
Chanzo: KPMG
Kando na
kutawala orodha ya 10 bora, kulikuwa na klabu nyingine tatu za Uingereza
katika orodha ya 20 bora - West Ham United, Leicester City na Everton.
SSC Napoli (nafasi ya 17) nao wamekuwa klabu ya pili kwa thamani Italia, nyuma ya Juventus lakini mbele ya AC na Inter Milan.
Haki miliki ya pichaReutersMwaka huu, klabu 12 zilikuwa na thamani ya zaidi ya euro bilioni moja, mbili zaidi ya 2017 ambapo zilikuwaklabu kumi pekee.
Na klabu sita zina thamani ya zaidi ya euro bilioni mbili, tatu
kutoka Ligi ya Premia, mbili kutoka Uhispania na moja ya Ujerumani.
Misimu
ya 2015-16 na 2016-17, Manchester United walishinda Kombe la FA, Kombe
la Ligi na Europa League. Lakini msimu huu wamemaliza bila kikombe hata
kimoja.
-
Zikiwa zimesalia siku 29 kufikia Tanzania iingie kwenye Uchaguzi wa
Rais,wabunge na nafiwanMkuu wa mwkaa 2020 Time ya Uchaguzi umekutana na
wadau wa mbalim...
0 Comments:
Post a Comment