AFISA ITIFAKI OFISI YA MKUU WA MKOA ARUSHA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMTEKA MWANDISHI


Afisa itifaki Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, Swalehe Mwidadi na mfanyakazi Ofisi ya masijala, Amina Mshana leo wakiwasilia mahakama ya wilaya ya Arusha 

Amina Mshana akiwa kwenye mahakama ya wazi ya wilaya ya Arusha akisubiri kusomewa mashitaka yanayomkabili


Awali mwandishi wa Habari Lucas Myovela aliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari akidai watuhumiwa hao Kwa pamoja  walimteka, kumtisha Kwa silaha na kumdhalilisha kwa kumvua nguo kisha kupiga picha.



OFISA itifaki (protocol officer) mkoani Arusha,( jina linahifadhiwa) anatuhumiwa kumteka, kumpiga na kumfanyia vitendo vya udhalilishaji mwandishi wa habari wa  kujitegemea, Lucas Myovela.
Aidha anadaiwa kumtisha kwa silaha, bastola na jambia huku wakimrekodi picha za utupu (video) ambapo walifanikiwa kuchukua fedha taslim elfu 75 alizokuwa nazo pamoja na kiasi kingine kutoa kwenye akaunti yake ya M Pesa.
Baada ya kukamilisha nia yake, ofisa itifaki huyo akisaidiana na watu wengine watatu anadaiwa kumpeleka Myovela kwenye kituo cha kati cha polisi na kudai kuwa ni jambazi aliyetaka kuwaibia gari.
Akiongea na waandishi wa habari nje ya kituo kikuu cha kati cha polisi Arusha, Myovela alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku baada ya kupigiwa simu na mfanyakazi wa kike kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa, (jin linahifadhiwa).

Alidai mwanamke huyo aliwahi kuwasiliana naye siku za nyuma akimuomba amsaidie kupata watetezi wa kisheria kwani alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na ofisa itifaki huyo ambapo hataki kuendelea nayo kutokana na manyanyaso ya kupigwa.

Myovela anadai kuwa manamke huyo alimweleza kuwa ofisa itifaki huyo alimnunulia samani za ndani na vitu vingine ambavyo yuko tayari kumlipa ili waweze kuachana ambapo jumapili majira ya  saa 10 mwanamke huyo alimwambia amepata ushahidi wa sauti aliyomrekodi ofisa itifaki juu ya suala hilo hivyo ni muhimu wakaonana.

Anadai alimjibu kuwa kwa wakati huo hawataweza kuonana kwani alikuwa Moshi Mkoani Kilimanjaro akishughulikia matibabu ya Baba yake mzazi ambapo alimtaka akirudi Arusha wawasiliane.

Myovela alisema kuwa Amina alimpigia simu majira ya saa tatu usiku akimsisitiza ni muhimu waonane ambapo Myovela aliamua kuchukue usafiri wa pikipiki kutoka USA River maeneo ya Nelson Mandela anakoishi mpaka  Ngulelo alipotakiwa kukutana na Amina.

“Nilipofika nilimkuta yupo kwenye gari lake akaniambia kaa, nikakaa kwenye kiti cha mbele mguu mmoja nimeweka chini ili nimsikilize. Akawa anaendelea kuchat kupitia simu yake ya kiganjani lakini akawa ananiambia ndiyo ananitafutia hiyo sauti nikusikilizishe haikupita hata dakika tano akaja ofisa itifaki huyo na watu wengine watatu, ambapo wengine walikuwa ameziba sura zao kwa 'mask' usoni,".

"Wakishirikiana na (ofisa itifaki) walinifunga kamba iliyopita kichwani, shingoni wakanishika yule binti akauliza twende wapi wakasema twendeni Sakina wakaniambia tulia hivyo nikawa nimetulia tulipofika Sakina sehemu waliyopaki gari ni pambezoni mwa daraja,".

"Baada ya hapo wakaanza kunipiga kwenye gari 'wakanisearch' wakanivua sweta, simu zangu zote wakachukua, wakanitupia kwenye daraja bahati kule chini kulikuwa na maji nimeumia mguu tu wakazunguka wakaja na ndoo wakati huu mimi fahamu zangu kama hazipo sawa,".

"Wakanivuta mpaka nje ya daraja wakaanza kunipiga wakanitoa suruale nikabaki na vesti pamoja na boxer, wakanirudisha tena kwenye maji kama dakika 40 mpaka saa saba  kasoro usuku, wakaniamba wanataka laki 5, kwa sasa hizi hela ulizo nazo tunachukua zote nilikuwa na elfu 75 kwenye siku una shilingi ngapi wakaniambia toa pass word,".

"Walikuwa na kitu kama jambia na kitu kama bastola wakaniamba tofauti na hapo ubongo tunautawanyisha nikawapa password ya mpesa wakaangalia salio wakajirushia na ushahidi uko kwenye simu yangu hata jana nimeaonyesha hapa polisi,"

" Wakaniambia niwabe password ya kadi ya benki nikawaambia sikumbuki mpaka nikaangalie kwenye note book yangu wakatoa hiyo jambia wakaniambia hatuna haja hata ya kukukata vua hiyo boxer nikabakia uchi wakanza kunirekodi nikiwa uchi wakaniambia hizo hela zilizoko hapa kwenye akaunti yako zote tunachukua,". 
"Akaniambia tofauti na hapo tunataka laki 5 kufikia kesho (jumatatu) jioni nikawaambia sawa haina tatizo wakaniambia tofauti na hapo hizi video tunazozirekodi tutazitupia mitandaoni hiyo kesho jioni nikawaambia sawa,"
" Mmoja akasema tumchuke tumfungie kwenye mawe huku mtoni mwingine akasema hapa tumtafute askari wakataja kama majina ya askari wawili wanipe kesi basi wakanirudishia suruale yangu nivae kwa sababu boxer walikuwa wameshaichana,". 

"Wakaniambia tembea kwa miguu sisi tunakufuata nyuma kwa gari sikwenda umbali mrefu nikaanguka mwili ulikuwa umeisha nguvu.Akashuka jamaa mmoja mimi nikawekwa siti ya nyuma ofisa itifaki huyo alikuwa amekaa mbele wakaja mpaka kituo cha polisi Ngarenaro kikawa kimefungwa ndipo wakanileta hapa Central,".
Myovema anasema baada ya kufika polisi  Central "Wakasema huyu jamaa alitaka kutuibia gari lakini hakuweza tumemuwahi, polisi wakawauliza mbona anavuja damu wakamwambia alikuwa anajaribu kukimbia ameanguka kwenye mto tukamshika,"/
Myovela alisema kuwa alikanusha madai hayo ya ofisa itifaki na wenzake kwa kujitambulisha kwa polisi sanjari na kutoa vitambulisho vyake vinavyoonyesha yeye ni mwandishi wa habari.

" Nikawaambia hawa wameniteka hata sasa tunavyoongea hizo simu zao zina video walizonirekodi wakisema wanataka fedha. Basi polisi akawaweka chini ya ulinzi akachukua simu zao ofisa itifaki akakimbilia kwenye gari kufuta video lakini yule mmoja wakadai aliondoka na simu yangu kubwa,".
"Baada ya polisi kumuona ofisa itifaki amejifungia kwenye gari wakamgongea akafungua mlango wakachukua simu walipoifungua wakaona video nzima ya namna walivyonifanyia unyama,".
Myovela alisema kuwa aliandika maelezo mpaka saa 11 alfajiri akapatiwa fomu malum ya polisi kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu (PF 3) ambapo alienda hospitali ya mkoa ya Mount Meru ndio akairjesha kituo cha polisi cha kati.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa kuwa kuna mtu alitembea na mke wa mtu hivyo akaweka mtego wa kumpata mtuhumiwa hivyo jeshi la polisi litafanya uchunguzi kubaini ukweli ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Hata hivyo hakuwa tayari kutaja majina ya mtu anayedaiwa kufumania wala kufumaniwa na mke wa mtu kwa kile alichodai kufanya hivyo ni kuingilia upelelezi.

Majira ya mchana siku ya Jumatatu ofisa itifaki huyo alionekana akiwa kwenye ofisi maeneo ya polisi akiwa  amefuatana na askari wa upelelezi hata hivyo haikujulikana mara moja endapo yuko chini ya ulinzi au la.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Arusha (APC), Claud Gwandu alisema kuwa kitendo cha kutekwa na kudhalilishwa Myovela ni kitendo cha kikatili ambacho akifai kufumbiwa macho.
“Naamini kuwa Lucas ameonewa, na hata kama anamakosa kulikuwa na taratibu ambazo zilitakiwa kufuatwa na siyo kuitwa usiku na kuanza kuteswa kwa kuwekwa ndani ya maji, kuvuliwa nguo,kupigwa picha na kunyang’anywa vitu vyake vitendo hivi havikubaliki," alisema Gwandu na kuongeza.
“Tunataka watu wote waliofanya hivyo wachukuliwe hatua kwa bahati nzuri, wanajulikana na siyo wale wasiyo julikana tunataka hatua kali zichukulie na wafikishwe kwenye mikono ya sheria”




0 Comments:

Post a Comment