SELASINI AMSHUKIA JPM



MBUNGE wa Rombo,  Joseph Roman Selasini, (CHADEMA), amemweleza Rais John Magufuli ambaye ni mkatoliki kuwa  kukataa kupokea maagizo ya kanisa ni sawa na kujitenga nalo.

Soma ujumbe wake kama ulivyo..


Mhe Rais jana nilikuona St Joseph's kwenye adhimisho la Pasaka. Wewe ni Mkristu Mkatoliki na Mseminari mwenzangu. Hivyo sina shaka ya  wewe kupokea ujumbe wangu huu kwa kuwa ni wa kiimani.
  Mhe Rais ktk kanisa tupokea na kuamini ktk DOGMA( Mafundisho ya Kanisa ambayo yanapokewa kwa imani na bila kupingwa).
   Zipo dogma nyingi tukianza na CREATION(Uumbaji) lakini mimi kwa muktadha huu nataka kuzungumzia moja tu nayo ni INFALIBILITY OF THE POPE na HIERARCHY ya kanisa.
Kanisa letu linaongozwa na ROHO MTAKATIFU anaetufundisha kupitia BIBLIA TAKATIFU, MAPOKEO na MAUNDISHO KUTOKA NYARAKA MBALIMBALI ZA KANISA( PAPAL BULLS) kila Mkatoliki anapaswa kushika yote kwa imani na kinyume chake ni kujitenga na Kanisa.
Papa anaongoza kupitia kwa waandamizi wake kuanzia CURIA(BARAZA LA VATICAN) SINODI ZA MAASKOFU WA MAENEO MBALIMBALI NA MABARAZA YA MAASKOFU.
      Waraka wa kichungaji ni moja kati ya nyenzo zinazotumika na kanisa kuwafundisha waamini. Baraza la Maaskofu kabla ya kutoa waraka wowote huujadili na kuupigia kura. Waraka unapita kama utapata kura asilimia sabini na tano ya Maaskofu wote. Kabla ya kuutoa Maaskofu hufunga na kuomba maongozi ya Roho Mtakatifu. Kisha waraka husajiliwa VATICAN ili uwe mali ya kanisa zima. Hivi ndivyo waraka unaoubeza ulivyopatikana na kutolewa kwa Waamini. Sisi Wakatoliki tunaamini hiyo ni kazi ya Roho Mtakatifu na sio kiwewe cha Maaskofu kinachotokana na kupungua kwa sadaka kama ulivyosema.
    Mhe. Kupingana na Waraka huu ni kuyakataa mamlaka ya kanisa na kazi ya Roho Mtakatifu ktk kuliongoza kanisa. Ni kuyakataa mamlaka ya Papa kama mkuu wa kanisa anaewateuwa na kuwaweka Wakfu na kazini Maaskofu kwa nguvu ya Upako wa Roho Mtakatifu.
   Hatua uliyochukua zamani na hata sasa tunaiita HERESY(UZUSHI) na ungetengwa na kanisa.
Nimeandika kukushauri kwa busara yako usigombane na maaskofu. Waamini tunawaheshimu na kuwaamini viongozi wa dini kuliko kiongozi yeyote wa Serikali wa ngazi yoyote. Ukifanya hivyo Taifa litagawanyika.
Pili tafuta njia isiyo wazi nyuma ya kamera au pazia uongee na viongozi hawa. Hawa sio Wanasiasa kama mimi ambao unaweza kuagiza tukafanywa chochote. Viongozi hawa wako tayari kufa kwa ajili ya kuilinda imani. Wanao mfano wa Yesu mwenyewe na Mitumi wake.
Tatu nakushauri uunde jopo litakalokuwa linakushauri mara kwa mara kuhusu mahusuano yako na viongozi wa dini wasio wanafiki na walioshika kwa ukamilifu imani zao kwa dini zote Waislam na Wakristu. UCHUMI WA KATI WA VIWANDA UNAOHUBIRI KAMWE HAUTAFANIKIWA KAMA NYUMA YA MAHUBIRI YAKO WAPO WATANZANIA WENYE MANUNGUNIKO NA WANAOUMIA NA KUTESEKA BILA KUSIKILIZWA, AMBAO VIONGIZI WA DINI WANAPOWASEMEA KAMA SASA UNAWABEZA.
ASANTE SANA,
Ndimi Mtumishi Mwaminifu wa Warombo,
.

0 Comments:

Post a Comment