BAADA YA KUTOKA SEGEREA,MBOWE ALISHUKIA BUNGE


KIONGOZI wa Kambi Rasmi  ya Upinzani Bungeni,  (KUB), Freeman Mbowe amelalamikia ofisi ya katibu wa bunge akidai inalenga kuua upinzani kwani wamewafukuza watumishi wote wa kambi hiyo.

Mbowe ameyasema hayo leo akiongea na waandishi wa habari mjini dodoma kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea bungeni na nchini kwa ujumla.

"Nimewaita kuzungumzia mamabo mawili, Kwanza kukosekana kwa maoni ya upinzani bungeni leo na pili uendeshaji wa kambi ya Upinzani Bungeni."

"Kanuni ya 16 (4) ya Bunge ndiyo iliyozaa Kanuni za kambi ya Upinzani, inaruhusu kambi kutunga kanuni zake"

"Bunge lina watumishi zaidi ya 400 lakini kambi ya upinzani inao 4 tu, huu ni mkakati wa makusudi kuhakikisha kambi rasmi inakuwa under staffig"

"Watumishi wa upinzani walifukuzwa na Katibu wa Bunge Januari kutokana na mikataba kumalizika Disemba"

"Nilipomfuata Katibu wa Bunge kumuuliza kulikoni unawafukuza hawa watumishi kama mbwa, akanijibu anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni. Ajira zao watumishi msubiri Spika. Hadi leo kambi haina hata mtumishi mmoja. Hatuna hata mtaalamu mmoja wa kuandaa hotuba na kuchambua nayaraka"

"Sasa kwa hali hii tunapata wapi taarifa ya kuwasilisha bungeni ?"

"Watumishi wa CCM hapa bungeni wapo na hawajafukuzwa kama wa kwetu"

"Alitegemea mimi niandae hotuba Segerea ambako hakuna sekretariet"

"Mikakati ya Katibu wa Bunge ni kuua upinzani. ndiyo jukumu alilokuja nalo"

"Baada ya kuona kuna tatizo kwa Katiba. Nilimwambia Spika anipatie kibali cha kuajiri lakini kanipa cha ajira 3. Hivi kweli watumishi watatu wasimamie wizara zote"

"Tangu Januari nimenyimwa hata Dereva.Tangu Januari sijatumia gari hilo la KUB na hawanipi stahiki zangu ambazo zipo kisheria"

0 Comments:

Post a Comment