#HuuSiUtanzania
Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa.
Nimetumia muda mwingi nikitafakari na kumfikiria sana mwanasiasa mwenzangu, kaka yangu, mbunge mwenzangu na rafiki yangu Tundu Antiphas Lissu.
Siku zote, katika maisha yetu ya kisiasa, hata katika mambo tunayotofautiana na kupingana nimekuwa nikiamini kwa dhati kwamba tofauti hizo haziwezi zikatufanya tukashindwa kuvuka salama kama Nchi, Kama Taifa.
Kilichotokea na kumpata ndugu yetu Lissu jana, ni kitendo cha kihalifu na kisichoendana kabisa na utamaduni wetu wa ustahimilivu na udugu ambao nchi yetu imekuwa ikisimamia.
Kitendo kile cha kikatili kinakwenda kinyume kabisa na misingi ya utaifa wetu ambao tumekuwa tukiujenga kwa miaka 25 sasa kwa kuwa na taifa huru kidemokrasia.
Wakati tukimuombea Lissu kupona kwa haraka, Watanzania tunaolitakia mema taifa hili tuna kila sababu ya kulaani na kukataa kabisa utamaduni huu wa kimafia kuzoeleka katika taifa letu.
Tusimame kulaani kwani #HuuSiUtanzania
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Septemba 8, 2017

0 Comments:
Post a Comment