![]() |
| Dereva wa Tundu Lissu anonekana kwenye Picha hii akiwa ameshikilia nguo za Tundu Lissu muda mfupi baada ya kupigwa risasi Tundu Lissu. |
DEREVA wa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, (CHADEMA), ametakiwa afike polisi ili aweze kutoa maelezo kuhusiana na tukio la kupigwa risasi bosi wake.
Aidha Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Vicent Mashinji anatakiwa kufika kwa Mkuu wa Upelelezi, (RCO), wa Dar es Salaam au Dodoma kutokana kauli anayodaiwa kuitoa akidai kuwa katika uchunguzi wao wamewabaini wahusika.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, (RPC), Gilles Muroto kuwa mpaka sasa wamekata magari nane aina ya Nissan Patrol kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa risasi kwa Rais huyo wa Chama cha Mawakili nchini, (TLS), Lissu.
Amesema uchunguzi huo unafanywa kwa kuvishirikisha vyombo vingine vya Serikali ikiwemo Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA).

0 Comments:
Post a Comment