HABARI: Timu ya Polisi imepata Msaada wa Fedha na jezi kutoka SportPesa


KAMPUNI ya SportPesa imewapatia timu ya soka ya Polisi Tanzania vifaa vya michezo pamoja na fedha taslimu Sh. Milioni 20 .

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo wakati wa mabakidhiano hayo kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas Alisema wanatambua mchango wa jeshi la Polisi kwa jamii, kwa kuwa linafanya kazi kubwa kuhakikisha nchi na wananchi wanakuwa salama.
“Tunatanguliza shukrani za dhati kwa SportPesa kwa vifaa hivi pamoja na fedha hizi na tuna waahidi hatutawaangusha, kwani timu yetu ilikuwa na uhaba wa vifaa mbalimbali na fedha mlizotupatia zitaisaidia timu kutatua shida mbalimbali,” Alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro kwa niaba ya timu,
SportPesa ni kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ambayo pia inazidhamini klabu tatu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba, Yanga na Singida United.

0 Comments:

Post a Comment