Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Vincent Mashinji, akiambatana na wasaidizi wake kutoka Makao Makuu ya Chama, amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam, muda huu.
Afisa habari wa chadema, Tumaini Makene amesema hatua hiyo ni kuitikia wito wa Jeshi la Polisi uliotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto, kuwa anatakiwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

0 Comments:
Post a Comment