Rais Donald Trump wa Marekani na mwenzake Moon Jae-in wa Korea Kusini wamekubaliana kuongeza shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini.
Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza kwenye ikulu ya Marekani jana Ijumaa na baadaye kufanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.
Trump alisema mipango ya nyuklia na makombora ya Korea Kaskazini inahitaji jibizo madhubuti. Aliongeza kuwa zama za uvumilivu wa kimkakati dhidi ya Korea Kaskazini zimekwisha.

0 Comments:
Post a Comment