Kufuatia baridi kali Arusha Diwani Melance Kinabo wa Kata ya Themi amesema leo ameamua kutembelea wananchi ikiwa ni pamoja na kutaka kujua kero mbalimbali katika kata yake lakini pia kuwajulia na kuwatembelea wazee ambao wapo kwenye kata hiyo ambao hawajiwezi.
Mh. Kinabo ameitembelea Kaya saba (7) ambapo amegawa Blanketi 1 , shuka 2, na Foronya 3 kwa kila familia aliyoifikia.
Diwani Kinabo amesema kipindi hiki kumekuwa na Baridi kali kiasi ambacho vikundi vya wazee katika jamii hawatoweza kumudu hali hiyo. hivyo akaamua kutoa msaada huo kwa familia kadhaa.

Aidha Kinabo ameeleza kuwa msaada huo utakuwa endelevu katika kata yake ambapo atawatembelea wazee wengine zaidi ili kuweza kusaidia kwa kiwango chake.
Leo Diwani huyo wa Themi kwa tiketi ya CHADEMA Ametembelea mtaa wa Kambarage na kuwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi na utendaji wake wa kazi.

"Nimeshawishika kutoa msaada huu kutokana na hali ya baridi kuwa kali zaidi katika jiji la Arusha , ziara yangu ya leo ilikuwa kuwatembelea wazee na kuwapa msaada huo" Mh. Kinabo alisema
Pamoja na kutoa misaada hiyo Diwani huyo ameeleza kuwa amegundua kuwa wazee wanakumbwa na matatizo mengi hasa magonjwa . ambapo ameahidi kuwasaidia wale amabao amewakuta wakisumbuliwa na magonjwa kwa kuwapeleka matibabu.
Wazee wanaopewa msaada huo ni wazee ambao wanaishi katika mazingira magumu kimaisha , Bw. Kinabo amewakabidhi msaada huo Bibi Mariam, Mzee Paskali William , Andrea Lukuwi , Bibi Agness Paka, Mama Shila na Bibi Mwadawa wote wakazi wa Mtaa wa Kambarage katika Kata ya Themi.
Katika hatua yingine Kinabo amekagua mradi wa Maendeleo wa Daraja linalojengwa katika mtaa wa Kambarage. Daraja ambalo linaunganisha Kata ya Themi na Kata ya Engutoto mkoani Arusha.
"Nimekuja pia kutembelea mradi wa Kivuko cha hapa Kambarage mradi ambao tumejenga kwa ufadhili wa watu tofauti tofauti lakini tunashukuru umekamilika, na kama mnavyoona umebakia tu hatua za mwisho za kuweka Paving Blocks" Aliongeza Mh. Kinabo

KUHUSU MIRADI YA MAENDELEO THEMI

![]() |
| Muonekano wa Daraja la Kivuko cha Mtaa wa Kambarage kati ya kata ya Themi na Engutoto. Picha ya VOA TV |

0 Comments:
Post a Comment