KIMATAIFA: Uturuki yaikemea ujerumani mkutano wa G20


Msemaji wa Rais İbrahim Kalın amekemea na kutounga mkono uamuzi wa Ujerumani kumkataza rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan kuhudhuria mkutano wa G20 akiwa na walinzi wake.
Ujerumani inaendelea kuchukua hatua ambazo zinakiuka uhuru na haki za kibinadamu
.Berlin inamtaka rais Recep Tayyıp Erdoğan kutoambatana na walinzi wake wakati atakapohudhuria mkutano wa G20 nchini Ujerumani
.Ankara imekosoa vikali hatua hii .Msemaji na mshauri wa rais İbrahim Kalın amesema kwamba hawatokubali hatua na nia mbaya za baadhi ya wanasiasa wa Ujerumani
.Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki naye pia amafahamisha kwamba  hesabu za ndani za Ujerumani zinakemewa vikali huku waziri wa EU nchini Uturuki akifahamisha kwamba hatua za Ujermani hazionyeshi ulinzi wa uhuru bali zinaonyesha ukosefu wa heshima kwa uhuru.

0 Comments:

Post a Comment