YALIYOMO KATIKA MUSWADA WA SHERIA YA FEDHA WA MWAKA 2017 KIKAO CHA 53 MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 LEO TAREHE 22 JUNI, 2017.



Lengo la muswada huu kufanyia  marekebisho sheria mbalimbali za kikodi na nyinginezo ili kuwezesha utekelezaji wa kisheria wa Bajeti ya Serikali wa mwaka 2017/18-Mhe. Dkt. Mpango

Muswada huu unakusudia kuzifanyia marekebisho Sheria kumi na tano-Mhe. Dkt. Mpango

Muswada huu unakusudia kupunguza kiwango cha ushuru wa bidhaa kwa baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini.-Mhe. Dkt. Mpango

Muswada huu utaweka utaratibu wa kudhibiti utoaji wa madini migodini kwa ajili ya usafirishaji nje ya nchi au kwa matumizi ndani ya nchi-Mhe. Dkt. Mpango

Kupanua wigo kwa kutoa fursa kampuni,watanzania wanaoishi nje ya nchi,taasisi za nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kununua hisa za kampuni za mawasiliano-Mhe. Dkt. Mpango

Kuweka utaratibu wa kuwatambua rasmi,washereheshaji kwenye sherehe, watoa huduma ya chakula, wafanya biashara wadogo wasio rasmi kwa kuwapatia vitambulisho maalum vya kazi-Mhe. Dkt. Mpango

Muswada huu kwa kiwangi kikubwa umezingatia mawazo na mapendekezo ya wadau mbalimbali wakiwemo wabunge,wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda, na taasisi binafsi na za Serikali-Mhe. Dkt. Mpango

Muswada huu utapunguza kiwango cha ushuru kwa bidhaa zinazozalishwa nchini-Mhe. Dkt.Mpango

Kutoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani kwa magari yanayotumika kwa ajili ya kubeba wagonjwa-Mhe. Dkt. Mpango

Muswada huu utapunguza ushuru wa mazao unaotozwa na halmshauri za Wilaya kutoka kiwango cha asilimia 5 ya thamani ya mauzo hadi asilimia 3 kwa mazao ya biashara-Mhe. Dkt. Mpango

Muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2017 (The Finance Act 2017) umepitishwa na Bunge jioni hii.


IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI- (MAELEZO)

0 Comments:

Post a Comment