Yeni Åžafak:Tumekuja hapa kupata suluhisho
Wajumbe wa wizara ya mambo ya nje wakiongozwa na waziri Mevlüt Çavuşoğlu wamehudhuria mkutano wa kutatua mzozo wa Cyprus unaofanyika Crons-Montana nchini Uswizi .Huku kukiwa na historia ya unyama katika mzozo huo wa Cyprus,waziri Çavuşoğlu alitoa ujumbe katika siku ya kwanza ya kongamano hilo.Çavuşoğlu kwanza kabisa alibainisha kwamba wameenda hapo kutafuta suluhu na kusisitiza kwamba Uturuki inapendekeza zaidi kuwe na suluhisho la kisiasa la kudumu na la haki .
Gazeti la Habertürk:Bandari salama zaidi duniani nchini Uturuki
Rais wa jamhuri ya Uturuki kupitia akaunti ya mitandao ya kijamii amesema kwamba siku za mbeleni zitakuwa bora zaidi kwa Uturuki hasa upande wa soko la fedha na uig,aji wa fedha nchini.Aidha alifahamisha kwamba Bülent Gedikli ni bandari ambayo ipo salama zaidi duniani ambayo inapatikana nchini Uturuki.
Gazeti la Hürriyet :Waturuki pekee ndio watafanya kazi nchini Qatar
Sheikh Abdulaziz bin Ahmed Al Thani, ni mojawapo ya wanachama wa familia ya Al Thani ambayo ni wamiliki wa kampuni maarufu na kubwa zaidi ya Sharaka Holding ambayo inahusika na masuala ya ujenzi Qatar.Al Thani imefahamisha kwamba haitojihusisha tena na Muungano wa mataifa ya Ghuba (GCC) na kwamba watafanya ushirikiano wa kikazi na Uturuki.Sheikh Abdullah alielezea kwamba hatua Saudi Arabia na mataifa mengine ya ghuba kuwekea vikwazo Qatar ilikuwa huzuni kuu na matumaini kukatwa.Aliendelea kufahamisha kwamba sasa Qatar itakubali bidhaa kutoka Uturuki,kutoka mataifa mengine ya Kiarabu na pia kutoka Afrika .Aidha Abdullah alifahamisha kwamba Qatar aitapeleka bidhaa nyingi za kutosha za sekta ya afya na pia sekta ya Ujenzi nchini Uturuki.
0 Comments:
Post a Comment