“Kila mtu ana mtazamo wake, na huwezi kulazimisha mtazamo wa mtu ubadilike. Inasikitisha sana kuona mtu anayesambaza haya mambo ni bosi wangu, Bosi wa mkoa wetu. Yeye akipiga mhuri kitu ndio imekaa hiyo, Yeye ana nguvu zote,” amesema Ruge.
“Sasa akisema hivyo mimi ni tapeli anataka kila mtu Dar es Salaam anione hivyo. Mimi sina nguvu kwa hiyo nachagua kubaki kwenye ninacho kiamini. Tangu mwanzo nilisema mimi nataka haya mambo yaishe, cha kusikitisha huyu mtu ni kiongozi lakini anashindwa kumaliza jambo hili kwa busara na anataka kuliendeleza.
“Kuna mambo hapa yanajaribu kutengenezwa. Watu wanajaribu kutusukuma turudi kwenye mjadala ambao tulishaumaliza. Mimi ni mtu mzima , na busara inaniambia watu wazima hatuna haja ya kurudi kwenye majibizano ambayo kwangu yaliisha siku nyingi “alieleza Ruge.
0 Comments:
Post a Comment