MEYA ARUSHA: ' NAMWAMBIA RAIS KUNA MKAKASI SUALA LA RAMBIRAMBI ARUSHA"

Meya wa  Arusha Mh. Kalisti Lazaro
Kama tulivyoripoti hapo awali leo kulifanyika ibada Maalum ya ahukrani na kuwaombea Majeruhi na narehemu wa ajali ya Lucky Vicent. Ibada ambayo imefanyika katika Kanisa la KKKT Olasiti.

Ambapo kati ya mengi yaliyojiri ni pamoja na kuwaombea majeruhi na marehemu , ambapo wazazi waliofiwa nao walihudhuria katika ibada hiyo huku mmoja wa wazazi hao alifafanua mchakago wa namna shughuli ya rambirambi ilivyoendeshwa hadi kufikia wao kujitoa.

Mara baada ya Wazazi kujitoa katika kamati ya RC Gambo , ambayo imekuwa ikishughulika na mchakato wa kuhakikisha rambirambi zitumike namna gani.

Habari Tanzania Grace Macha Blog tulipata kuzungumza na Mmoja wa wazazi ambao wallikubwa na msiba ulioiaibu taifa baada ya gari la shule ya Lucky Vincent kupata ajali na kuondoka na maisha ya ndugu zetu Wanafunzi zaidi ya 30, dereva na waalimu walioambatana na wanafunzi hao katika gari liliopata ajali.
Wananchi waliohudhuria katika ibada hiyo

Katika mazungumzo Maalum na Mzazi huyo ambaye hakupendelea Jina lake lisitajwe ameeleza sababu ya hasa kwa nini wamejitoa katika kamati iliyoundwa na mkuu wa mkoa Mh. Mrisho Gambo

"Tuliona hakuna sababu ya kuwepo katika kamati ya maafa kwa sababu tuliona fedha za rambirambi haikuwa inatumika malengo husika, pia baada ya tukio la juzi 'Kukamatwa Viongozi waliopeleka rambirambi mbele yao'  baada ya hapo wafiwa waka hoji kwa nini rambi rambirambi zisitumike kwa malengo husika,  Kuhusu fedha za rambirambi zilizobaki Mzazi anaeleza kwamba " Tuliambiwa hizo fedha ziende hospigalini kwa kutumika katika maeneo ya ukarabati wa Muchwari, ICU na kutengeneza kitengo cha akili ." Alisema Mzazi
Mmoja wa wazazi waliofiwa ajali ya Lucky Vincent

Habari Tanzania Grace Macha ilimtafuta Meya wa jiji la Arusha baada ya wazazi hao kujitoa " Kwanza niahukuru kwa sababu leo nimetimiza azma yangu yakufanya ibada kwa ajili ya watoto wetu walioko marekani na marehemu , hii inadhihirisha kwamba tangu awali mkuu wa mkoa alikuwa hana kamati , hana akunti Maalum wala hana taratibu Maalum , wazazi hao wamejitoa kwa sababu hawaoni sababu ya kuwepo katika kamati hiyo kwa sababu shughuli nzima ilishakamilika" Alisema Meya

"Namwambia Mh. Rais kuna ukakasi kwenye suala la rambirambi Arusha na namna ambayo inaendelea kamati inaundwa kwa siri na kulazimishwa namna ya kufanya nini, wazazi hao wamejitoa, sasa naitaka mkuu wa mkoa , RAS, na mganga mkuu waamue matumizi ya hiyo hela sisi wananchi wa Arusha na viongozi wa kuchaguliwa na tunaungana na wananchi waliojitoa" alisema Meya Arusha

0 Comments:

Post a Comment