BURUDANI LEO: WCB kumtangaza msanii mpya Kesho

Diamond na Zari

Wakati Diamond Platnumz msanii anayefanya vizuri kimataifa na mkali wa wimbo 'Marry You' akishika headlines barani Africa kwa kuhudhuria Tamasha la KAROGA FESTIVAL Huko Nairobi nchini Kenya hapo May 28 Tamasha linalosubiriwa kwa hamu kubwa kama ilivyo kawaida ya msanii huyo kufanya matamasha yanayokonga nyoyo za wengi popote anapotangaza kufanya Tamasha.

Sasa msanii huyo anashika vichwa vya Habari za burudani nyumbani Tanzania Mara leo kutangaza kuwa kesho atakuwa na crew ya label ya muziki anayoimiliki WCB Wasafi katika Kipindi maarufu cha 'Leo Tena' ya Clouds FM kumtambulisha msanii mpya anayejiunga na label hiyo.

Diamond ameweka unumbe huu kwenye kurasa take ya Instagram 'From @diamondplatnumz  Panapo majaaliwa siku ya jumatatu kesho, ntakuwepo kwenye LEO TENA  ya Clouds fm na familia nzima ya @Wcb_wasafi tukimtambulisha Kijana mwenzetu Mpya ndani ya @Wcb_Wasafi..... Sisi ni vijana ambao tumekulia kwenye umaskini na bado tupo kwenye kupambana namna ya kujikwamua kwenye umasikini... na ndiomaana tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kila tukiona kijana yoyote mwenye nia na kipaji kumsaidia kwa kadri ya uwezo wetu, ili nae aweze kutambulisha kazi zake, na Pengine Mwenyez Mungu akimjaalia nae awe mkombozi kwenye Familia yake....Sio jambo Rahisi ni gumu, lakini kwa Sapoti yenu naamini tunaweza lifanikisha...Siku zote naomba mkunbuke WCB_Wasafi sio ya Diamond,  ni ya vijana wote wapambanaji...na ndiomaana kila siku nawaomba Muendelee kuniombea na Kunisapoti,  kwani Sapoti yenu ndio itayo nifanya hata kesho niweze kukuchukua wewe ama ndugu yako ili aje kukitambulisha kipaji chake na Mwenyez Mungu akijaalia kufikia Malengo...... USIKOSE kusikiliza Leo tena ya @Cloudsfmtz saa nne Asubuhi...Shukran🙏'"

0 Comments:

Post a Comment