NA GRACE MACHA, ARUSHA
VILIO
majonzi simanzi imetawala jiji la Arusha wakati miili ya watoto 33
waalimu wawili na dereva ulipokuwa ukipitishwa kuelekea uwanja wa Sheikh
Amri Abeid kwa ajili ya kuagawa.
Miili hiyo iliondolewa chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya mkoa ya Mount Meru majira ya saa 5 asubuhi ikiwa imebebwa na magari matatu ya jeshi la Wananchi wa Tanzania, (JWTZ).
Msafara huo uliotanguliwa na gari la matangazo na gari JWTZ aina ya land rover ulipitia barabara ya Afrika Mashariki kisha ile barabara kuu ya Arusha Moshi ndipo wakaingia barabara ya Middleton ulipo uwajani huo.
Maeneo yote waliyopita kulikuwa na wananchi waliojipanga pembeni ya barabara ambapo miili hiyo ilipokuwa ikipita kulisikika vilio kutoka kwa wananchi hao.
UWANJANI VILIO VYATAWALA
Wananchi waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walipaza sauti za vilio pale magari yaliyobeba miili ya marehemu ilipoingia.

Magari hayo yalienda moja kwa moja eneo lilipotengwa kwa ajili ya kuweka majeneza yaliyokuwa na miili hiyo ambapo zoezi kuishusha kwenye gari na kuweka kulingana na utaratibu lilifanywa na wanajeshi.
WENGI WAZIMIA
Watu wengi waliofika uwanjani hapo walikuwa wakilia kwa huzuni huku wengine wakipoteza fahamu ambapo walipewa huduma ya kwanza na madaktari kutoka hospitali ya mkoa ya Mount Meru, hospitali teuli ya Wilaya ya Karatu ya Lutheran na taasisi ya Steam ya Mennonite ya nchini Marekani .
Pia watu wa Chama cha Msalaba Mwekundu nao walikuwa wakisaidia kuwabeba watu hao na kuwapeleka kwenye eneo walipokuwa madaktari hapo ambapo wengine walilazimika kukimbizwa hospitali kwa magari ya kubebea wagonjwa.
Hali hiyo ilifanya magari hayo ya wagonjwa kuonekana yakiingia na kutoka uwanjani hapo muda wote kuanzia majira ya asubuhi mpaka mchana hata pale zoezi la kutoa heshima za mwisho lilipositishwa bado walionekana watu wengine wakipoteza fahamu.
Hali hiyo ilimsababisha Askofu wa EAG, Askofu , Leonard Mwizarubi, kuwaomba Mungu awaepushe na madhara wale wanaopata mshituko na matatizo ya moyo kutokana na msiba huo.
Alisema kuwa kila mwanadamu ana mambo matatu wakiwemo yale ya siri, ya wazi na ni mjinga kwenye eneo fulani hivyo akasema ni vema watu wakaacha kujivuna kwa kile alichodai kuwa inawezekana wewe unajivuna kujua hili mwenzio anajua kile.
UWANJA WAFURIKA MILANGO YAFUNGWA
Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza uwanjani hapo kuanzia majira ya saa 11 alfajiri ambapo ikipofika saa 3 asubuhi ilibidi polisi kufanya kazi ya kuzuia watu wasiingie kwani majukwaa yote yalikuwa yamejaa watu na eneo la katikati.
Hata hivyo hiyo haikuwakatisha tamaa baadhi ya watu kwani waliamua kuingia uwanjani hapo kwa kuruka ukuta.
Aidha wengine walionekana wakifuatilia tukio hilo kupitia vituo vya televisheni na radio zilizokuwa zikirusha tukio hilo mubashara.
Waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene amesema ni vifo hivyo ni mpango wa shetani jambo alilodai kuwa anatofautiana na wale wanaodai ni mapenzi ya Mungu.
Mawaziri wa Afya, Ummy Mwalimu na yule wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadium, Profesa, Joyce Ndalichako, walitoa pole kwa wafiwa wote huku wakiwataka wawe na subira.
RAIS WA KENYA AMTUMA WAZIRI WAKE
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, aliwakilishwa na
Waziri wa Elimu wa Kenya, Dr Fred Matiani, ambaye aliwapa pole wafiwa na Tanzania kwa ujumla huku akiwahakikishia kuwa kama Taifa wapo pamoja nasi katika wakati huu maombolezo.
KINANA AIBUKIA MSIBANI, AUNGANA NA MBOWE WALILIA UMOJA WA KITAIFA
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Freeman MBOWE ndiye aliyeanza kuzungumza uwanjani hapo ambapo alisema kuwa Mungu amependa Watanzania wautumiea msiba huo kuutafakari umoja wao kupitia msiba huo.
Baada yake alifuatiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Abrahaman Kinana alisema kuwa jambo pekee linalowaunganisha Watanzania wote bila kujali tofauti zao ni msiba.
Viongozi hao waliwapa pole wazazi, waombolezaji na wananchi wote kutokana na msiba huo mkubwa
Kinana ameonekana hadharani kwa Mara ya kwanza kwenye msiba huo ikiwa ni zaidi ya miezi miwili sasa tokea Rais John Magufuli adai amemtuma kwa matibabu nchini India.
KAIMU JAJI MKUU
Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Hamisi Juma, aliwapa pole wafiwa huku akiwakumbushankuwa wanadamu wanapanga lakini Mungu ndiyo anaamua.
Alisema kuwa alisoma kauli mbiu ya shule hiyo inawataka kuwa mwanga hivyo walikufa wakiwa njiani kwenda Karatu kwenye mashindano ya kitaaluma kwa lengo la kuutafuta mwanga hivyo akadai mwanga waliokuwa wanautafuta duniani waendelee kuupata huko mbinguni
VIONGOZI WA DINI
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Nchini, (KKKT), usharika wa Arusha Kati, Solomon Masangwa, aliwatia moyo wafiwa ambapo aliwataka kila mmoja kujiweka tayari kwa kuwa hakuna ajuaye siku ya kuondoka hapa duniani huku akirejea maandiko matakatifu kutoka kitabu cha ufunuo wa Yohana 1:17-18
Akiongea kwa niaba ya Umoja wa Makanisa Arusha,
Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Josephat Lebulu aliwapa pole wafiwa akiimba wimbo toka kitabu cha
Zaburi sura ya 130 unaoswema " niinakulilia katika unyonge wangu ewe kinga yangu..
Sheikh Mkuu mkoa wa Arusha, Shaaban Juma alisema mwanadamu akishindwa kuhimili hasira shetani hutumia fursa hiyo kumuingia mwanadamu na kufanya uharibifu hivyo akashauri wafiwa kuzimiliki nafsi zao ili shetani asipate fursa ya kuwaingizia mawazo mabaya.
Hata hivyo alisema watu hawazuiwi kuhuzunika ila wawe na subira na waridhie kilichotokea huku wakiwaombea vijana hao waingie kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu.
Askofu wa Kanisa la Anglikana Daiyosisi ya mlima Kilimanjaro, Stanley Hotay, alisema vifo hivyo vimetikisa si Tanzania pekee bali na nchi za jirani hasa za ukanda wa Afrika Mashariki hivyo akafanya maombi kumuomba Mungu aepushe tukio kama hilo lisitokee tena.
MAKAMU WA RAIS AWATAKA MADEREVA KUWA MAKINI BARABARANI
Mkamu wa Rais, Samia Suluhu, akimwakilisha Rais John Magufuli, aliwataka alisema kuwa msiba ni wa aina yake na umewagusa Watanzania wengi hasa kutokana na ukweli kuwa malaika hao wameondoka dunia kwa matendo yasiyokuwa ya kwao kwani wao walikuwa njiani wanaenda kujifunza.
Alitoa wito kwa Wizarabya Elimu, Jeshi la Polisi, walimu na walezi na wazazi kuwa makini kuhakikisha kuwa sheria usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua kuwalinda watoto na wananchi wengine kwenye vyombo vya usafiri.
Alisema Taifa limepata pigo kubwa linalowakumbusha Serikali kufanya marekebisho ya mambo mengi yenye kasoro na yanayoleta maafa kama hayo.
"Naomba nitumie fursa hii nipaze sauti kuwaomba sana madereva kuwa na makini wanapokuwa barabarani, Serikali yetu inapiga vita utumiaji wa vilevi wakati mnapoendesha, tunapiga vita madawa ya kulevya kwa sababu tunajua hii ni moja ya sababu kubwa inayoleta hasara za namna hii," alisema na kuongeza.
"Kwa upande wetu Serikali tutajitahidi kuweka vizuri alama za barabarani, lakini na usalama wa barabarani ili kuepuka maafa ya namna hii.
" Lakini nizungumze tena na abiria wakati wanapochukua abiria wahakikishe kwamba magari wanachukua kulingana na uwezo yayotengenezewa," alisitiza Makamu wa Rais Suluhu.
Alimshukuru Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kumtuma Waziri wake wa Elimu kuja kujumuika kwenye msiba huo jambo alilosema kuwa inaonyesha undugu wa dhati kwa wananchi wa EAC.
"Walipopata ajali mbele yao kulikuwa na gari ya watalii ambao ni madaktari bingwa kutoka shirika la Steam, kutoka nchini Marekani, madaktari wale walisaidia eneo la ajali na kwa wale majeruhi watatu waliobakia madaktari hawa wamejitolea hata kuwapa matibabu ikibidi nje ya nchi," alisema Makamu wa Rais wakati akiwashukuru madaktari hao.
Alisema kuwa haipendezi kila mara kuwa na misiba inayotokana na ajali.
"Taifa lipo nanyi katika kipindi huki kigumu cha majonzi tele ni huzuni kwa Taifa na EAC giza limetanda nchini kote kama walivyosema viongozi wa dini tukubali hili limetokea.
"Habari za vifo hivi zimeleta huzuni na kufanya giza nene kutanda nchini, tumeelemewa na huzuni na majonzi tele lakini kwa kuwa kazi ya Mungu haina makosa Mwenyezi Mungu aliwapenda sana watoto wetu na kazi ya Mola haina makosa, "alisema huku akiwaomba wazazi kulikubali jambo hilo.
6:55 Makamu wa Rais aliondoka uwanjani.
WATOA HESHIMA ZA MWISHO WAKINYESHEWA NA MVUA KUBWA

Wakati zoezi la kutoa heshima za mwisho likiendelea mvua kubwa zilianza kunyesha lakini haikuzuia waombolezaji waliendelea na zoezi hilo huku wakiendelea kulowa.
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walijaribu kukimbilia jukwaani na maeneo yaliyokuwa yamefungwa maturubai kwa ajili ya kujikinga.
Aidha wengine walikuwa wakikimbilia ilipokuwa imewekwa miili ya marehemu jambo lililowafanya polisi na wanajeshi kufanya kazi ya ziada ya kuwazuia na kuwaondoa wale waliokuwa wamejipenyeza na kusimama eneo hilo.
WENGINE WARUDISHWA CHUMBA CHA KUHIFADHI MAITI
Miili ya marehemu ilianza kuondoka uwanjani hapo majira ya saa mchana ambapo mwili wa kwanza kuondoka ulikuwa ni wa mwalimu Innocent Papiani ambaye anapelekwa Kyerwa mkoani Kagera kwa ajili ya maziko.
Miili mingine iliendelea kuchukuliwa na familia zao kwa ajili ya taratibu za maziko kwenye maeneo mbalimbali kulingana na taratibu za familia zao.
Aidha miili inayokadiriwa kufikia saba ilirejeshwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ambapo wanatarajiwa kuzikwa siku zijazo kulingana na taratibu za familia zao.
SERIKALI YAGHARAMIA MSIBA
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema kuwa Serikali imetenga milioni 80 kwa ajili ya msiba huo ambapo kila familia itapatiwa sh milioni 1 na fedha nyingine zimetumika kwa ajili ya maandalizi ya uwanja kiasi cha Shilingi milioni 8, kusafirisha miili ya marehemu na familia zao shilingi milioni 27 na shilingi milioni 9 zikitumika kutengeneza majeneza yote.
Hata hivyo wakati akiwa uwanjani hapo wadau wengine walijitokeza kutoa rambirambi zao za fedha wakiwemo wabunge waliotoa shillingi milioni 100 na taasisi nyingine za kitaifa na kimataifa ambapo aliahidi fedha hizo zitagawanywa kwa familia zote
.
Baadhi ya waliochangiaji wengine ni pamoja na wabunge wa CHADEMA, Umoja wa Wanawake wa CCM, (UWT), Umoja wa bodaboda, Umoja wa makanisa Arusha na Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EAC).
Viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Meya wa jiji la Arusha Calist Lazaro, mawaziri, wakuu wa mikoa, wabunge, wakuu wa Wilaya na madiwani wa jiji la Arusha.

0 Comments:
Post a Comment