HABARI: PICH/AUDIO ni Sentensi muhimu za RC Gambo kuhusu Mbunge Lema na Meya Arusha

RC Mrisho Gambo

"Kwa kauli zao wenyewe wakikiri kwamba hawafahamu lolote kuhusiana na uratibu mzima wa maafa ambayo yaliiukuta mkoa wetu. Sasa ukizingatia kwamba kama mkoa kupitia Arusha Mjini tumepata pigo sana kutokana na vifo vya watoto wetu
Tumefurahi pia kuona watu wengine wanahitaji kupata taarifa kamili kuhusiana na namna ambavyo tuliendesha kwa mafanikio makubwa zoezi la kuhakikisha. AUDIO IPO HAPO CHINI BOFYA KUSIKILIZA



Nimefurahi kuona na wao pia kama watu wengine wanahitaji kupata taarifa kamili kuhusiana

 Namna tuliendesha kwa mafanikio makubwa zoezi la  kuhakikisha miili ya watoto inazikwa salama pamoja na watoto wetu wengine wanapelekwa kwa matibabu Marakani.

Kitendo cha wao kukiri hawajui chochote ninishara kwamba wamekubali sasa na wako tayari kuwa chini ya Serikali ya awamu ya tano niwaombe tu waendelee kuwa watulivu kwa sababu Serikali ya awamu ya Tano ni Serikali ya uwazi ni serikali ya ukweli ni serikali ambayo imedhaminiria kuweka heshima ya uongozi katika nchi hii tutaweka taratibu zote za msingi kwa jamii ili watu waweze kufahamu namna gani kama Serikali tumejitoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha changamoto hiyo kubwa iliyoukumba mkoa wetu na Taifa kwa ujumla inakamilika salama.

Nitumie fursa hii kuendelea kumuomba mheshimiwa Mstahiki Meya na Mheshimiwa Mbunge waendeelee kuwa watulivu waendelee kuwa wasikivu na sisi  tumedhamiria kuhakikisha kwamba tunawapa elimu ya uongozi unaoacha alama" RC Gambo

0 Comments:

Post a Comment