Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in amefanya mazungumzo ya simu na Rais Donald Trump wa Marekani mara tu baada ya kuapishwa. Walikubaliana kushirikiana kwa karibu katika kutatua masuala ya mipango ya nyuklia na makombora ya Korea Kaskazini.
Maofisa wa nchi hizo mbili wamesema Rais Moon na Rais Trump walizungumza kwa takribani dakika 30 jana Jumatano. Mazungumzo hayo ya simu yalikuwa ni ya kwanza kufanywa na rais mpya wa Korea Kusini kwa kiongozi mkuu wa nchi nyingine.
Ofisi ya Rais ya Korea Kusini imesema kuwa wakati wa mazungumzo hayo, Moon alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ili kushughulikia kuongezeka kwa hali ya wasiwasi juu ya usalama kwenye eneo la Rasi ya Korea.
Rais Trump alimpongeza Rais Moon kwa kushinda uchaguzi. Alimueleza Rais Moon kuwa suala la nyuklia la Korea Kaskazini ni tatizo gumu lakini linaweza kutatulika.
Rais Trump pia alimualika Rais Moon kutembelea Marekani kwa ajili ya mkutano baina ya viongozi hao katika siku za hivi karibuni. Moon ameripotiwa kukubali mwaliko huo.

0 Comments:
Post a Comment