1- Cape Town (South Africa)
Hili ni jiji la kwanza kwa uzuri Afrika, pia ni mji mkuu wa South Afrika na limekuwa na mvuto wa kipekee na kuifanya Afrika Kusini kuwa na hadhi ya kipekee ikiwemo kuongeza idadi ya watalii wanaofika kutembelea kwenye jiji hilo kila wakati.
2- Cairo (Egypt)
Kwa kiasi kikubwa jiji la Cairo limetawaliwa na Mahoteli ya kisasa, Misikiti mikubwa, Mapiramidi na sehemu za kihistoria.
3- Johannesburg (South Africa)
Huu ni mji muhimu kibiashara kwa Afrika Kusini, unawakilishwa na aina za majengo ya kisasa na marefu huku wengi wakilifananisha na jiji la Manhattan kutokana na urefu wa majengo yake.
4- Alexandria (Egypt)
Alexandria ni moja kati ya majiji yenye mvuto wa kipekee barani Afrika pia ndio jiji kongwe kuliko yote Afrika! Nchi ya Misri imekuwa ikifanya maboresho ya jiji hilo kila wakati ili kuendana na hadhi ya kisasa.
5- Bata (Equatorial Guinea)
Kwa kiasi kikubwa jiji la Bata linaongezewa mvuto zaidi na fukwe za bahari ambazo hujaa watalii na wapenda starehe.
6- Tunis (Tunisia)
Moja kati ya vitu vinavutia kwenye jiji hili ni hali ya hewa, sio joto sana sio baridi iko katikati. Tunis inasifika barani Afrika kwa mpangilio mzuri wa barabara zake pia mpangilio wa majengo yake.
7- Nairobi, Kenya
Wakati mwingine Nairobi huitwa Montreal of Africa, Nairobi ndio jiji lenye makao makuu ya taasisi nyingi za kimataifa.
8- Marrakech (Morocco)
Marrakech ni mji wa ndoto kwa watu wengi kutaka kuutembelea barani Africa. inapatikana katikati ya nchi ya Morocco, miaka ya nyuma paliwahi kupewa jina la Red City.
9- Dar es Salaam
Dar es Salaam ikiwa na maana ya Bandari ya Salama kutoka lugha ya Kiarabu. huu ndio mji muhimu wa nchi ya Tanzania na ndio jiji lenye watu wengi pamoja na shughuli nyingi zaidi Tanzania. Majengo mapya yanayojengwa kila wakati yanazidi kuifanya Dar es salaam izidi kuwa na mvuto.
10- Abidjan (Ivory Coast)
Abidjan inatajwa kuwa ndio sehemu muhimu zaidi kwa uchumi wa nchi ya Ivory Coast na ni sehemu yenye kutembelewa na watalii kwa kiasi kikubwa sana kwenye nchi za Africa.
0 Comments:
Post a Comment