WATU 19 wamefikishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arusha na kusomewa mashtaka 30 tofauti ya mauaji, kujaribu kuua, kula njama na kufanya vitendo vya kigaidi, kufadhili kufanyika kwa matendo ya kigaidi, kusambaza zana za ugaidi, kushawishi na kufadhili watu kujiunga na kundi la kigaidi la Al Shabab.
Aidha watu hao wanahusishwa na matukio ya mabomu kwenye mkutano wa Chadema, milipuko kwenye nyumba za mashekh, Abdulkarim Jonjo na Sudi Ally Sudi sanjari na kuwamwagia tindikali Mustafa Kiago, Halidi Mustafa kwenye msikiti mkuu wa Ijumaa na Shekh Saidi Mkamba.
Watu hao walisomewa mashtaka yao jana na wanasheria wa serikali, Agustino Kombe, Felix Kwelukira na Marselino Mwamunyange mbele ya hakimu mkazi, Devote Msofe aliyesikiliza kesi zao nane kuanzia namba PI 51mpaka PI58 za mwaka 2014.
Washtakiwa 12 walisomewa shtaka la kula njama na kufanya vitendo vya kigaidi kinyume cha sheria ambapo ilidaiwa kati ya januari na februari mwaka huu walikula njama na kufanya matendo ya kigaidi ambapo Julai 3, mwaka huu maeneo ya Majengo Chini walitupa bomu la kurushwa kwa mkono na kumjeruhi Sudi Ally Sudi na Yusuph Husein huku wakihatarisha maisha yao.
Aidha washtakiwa Jafar Lema, Hassan Mfinanga na Yusuph Ramadhani walidaiwa kuwa walitoa fedha kuwezesha kufanyika kwa vitendo vya kigaidi nyumbani kwa shekh Sudi.
Washtakiwa hao 12, walisomewa mashtaka manne ya mauaji ya na tisa ya kujaribu kuua ambapo ilidaiwa kuwa juni 15, 2013 kwenye viwanja vya Soweto waliwaua, Judith Moshi, Ramadhan juma, Fahar Jamal na Amir Dafa huku wakijaribu kujaribu kuua wengine tisa.
Wanasheria hao waliieleza mahakama hiyo kuwa washtakiwa wengine saba wanahusika na kukusanya zana kwa ajili ya kufanya vitendo vya kigaidi kinyume cha sheria ambapo kati ya kulai 23 na 30 mwaka huu huko maeneo ya Ngusero walikusanya mabomu saba ya kutupwa kwa mkono na risasi sita za short gun.
Aidha wanadaiwa kusambaza zana hizo kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kigoma kwa lengo la kutekeleza matukio ya kigaidi.
Pia, Ibrahim Leonard, Auar Hayae na Yasin Shaba wanashtakiwa kwa kufadhili na kushawishi vijana tisa kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Alshabab.
Hata hivyo washtakiwa hao hawakurusiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na nguvu ya kisheria kusikiliza mashauri hayo ambapo yameahirishwa mpaka Agosti 15, mwaka huu yatakaporudi mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.
Aidha washitakiwa kwenye mashauri hayo ni Yusuph Hussein Ally maarufu kama Huta (30), na mke wake Sumaiya Yusuph Hussein Ally (19) ambapo walikuwa na mtoto wao mdogo Yasir mwenye umri wa miezi 10.
Ramadhan Hamad Wazir (28),Hassan Ally Mfinanga (57), Abashar Hassan Omar (24), Kimoro Issa Mchana jina maarufu Omar au Abuu Twalib (25) Hassan Abdallah Omar (40).
HakiElimu Yaiomba Serikali Kuboresha Usawa Kati ya Shule za Kiswahili na
Kiingereza
-
Mkurugenzi wa HakiElimu Dkt John Kalage akizungumza na waandishi wa habari
leo Novemba 20, 2024 katika Ofisi za HakiElimu Jijini Dar es Salaam
NA EMMAN...
1 hour ago
0 Comments:
Post a Comment