Katibu Mkuu Dk. Slaa leo ataongoza waombolezaji katika mazishi ya
aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA Jimbo/Wilaya ya
Muheza, Kamanda Rashid Mwengo Mhina aliyefariki jana akiwa hospitali
ya Muheza, mkoani Tanga akiwa amewahishwa hospitali hapo kupata
matibabu baada ya kudondoka ghafla katikati ya shughuli ya uchaguzi wa
wilaya hiyo alipokuwa akijibu maswali ya wapiga kura, ambapo yeye
marehemu alikuwa akigombea nafasi ya uenyekiti wa Baraza la Wazee na
mweka hadhina wa wilaya.
Hadi mauti yanamkuta Kamanda Rashid alikuwa pia ni Mwenyekiti wa
CHADEMA Kata ya Magila.
Mazishi hayo yatakayohudhuriwa na Katibu Mkuu, yatafanyika leo
kitongoji cha Kwekiosi, Kijiji cha Mikwamba, Kata ya Magila baada ya
swala ya adhuhuri.
Mwenyezi Mungu aiweke mahali pema roho ya marehemu na awatie nguvu
familia katika wakati huu mgumu wa majonzi ya kuondokewa na moja ya
nguzo muhimu.
Mwenyezi Mungu pia awatie nguvu ndugu, jamaa, marafiki, viongozi
wenzake na wanachama wote wa Chadema kwa kuondokewa na mpiganaji
mwenzao.
Makene
TRA YAZINDUA DAWATI MAALUM LA UWEZESHAJI BIASHARA KWA MASUALA YA FORODHA
KWA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO
-
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua dawati maalum la uwezeshaji
biashara za Forodha kwa wafanyabiashara wa Kariakoo pekee ili kuharakisha
upatikanaj...
2 hours ago
0 Comments:
Post a Comment