MBOWE AWAONYA WASAKA MADARAKA CHADEMA

MWENYEKITI wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe akisimkwa kuwa Laigwanan na wazee wa mila za Kimaasai kwenye kata ya Nduruma
 
MBOWE akipeana mkono na wazee wa mila wa kimaasai mara baada ya kumsimika kuwa Laigwanan
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema akizungumza kwenye mkutano huo alisema kuwa Taifa lina rasilimali nyingi lakini amekosekana kiongozi mbunifu na makini wa kuzitumia kuboresha maisha ya wananchi wake.

"Rais (Jakaya Kikwete) anaacha mbuga za wanyama, gesi, dhahabu na tanzanite anaenda Marekani kuomba chandarua, hapa ndipo tunasema hakuna umakini," alisema Mjumbe huyo wa kamati Kuu ya Chadema.
 KATIBU wa Chadema kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa akizungumza kwenye mkutano huo pamoja na mambo mengine alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kwenye vikao mbaalimbali ili wapate taarifa za msingi kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Freeman Mbowe, ameonya kuwa chama chake hakitasita kumnyang'anya kadi mwanachama wake yeyote atakayethibitika kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa lengo la kujenga ushiwishi wa kukubalika kwenye chaguzi.

Aidha amewataka wale wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa tiketi ya chama hicho kwenye chaguzi mbalimbali kuelewa kuwa lengo la chama hicho ni kupigania maslahi ya wanyonge na si kutafuta ulaji.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, aliyasema hayo juzi wakati akihutubia wananchi kwenye viwanja vya Unguuni, kata ya Nduruma wilayani Arumeru.
Alisema kuwa kumekuwa na mwamko mkubwa miongoni mwa wanachama wa chama hicho kuonyesha nia ya kutaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye chaguzi zijazo kuanzia zile za Serikali za mitaa jambo alilowataka wasiwagawe wanachama ili kutimiza malengo yao kisiasa bali washiriki kujenga chama.

Mbowe alilazimika kuwapandisha jukwaani baadhi ya wanachama wa chama hicho walioonyesha nia ya kugombea ubunge jimbo la Arumeru Magharibi ambapo mpaka sasa wamefikia 14 akiwemo diwani wa kata ya kata ya Olturoto, Gipson Ole Meiseiyeki.




"Chadema hatugombei vyeo tunagombea maslahi ya wananchi, na muelewe mtu atachaguliwa kwa uchapakazi wake wala si fedha zake, na tukiona inafaa tutawatawanya kwenye mikoa mbalimbali kila mmoja akafanye kazi ya kujenga chama, tuwapime kwa historia zenu. Chadema hatuhitaji kujaza namba Dodoma (bungeni) tunataka mashine za kufanya kazi ," alisema Mbowe huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza kwenye viwanja hivyo.
Aliwataka wananchi kushindana kwa kupigania rasilimali za umma zitumike kwa manufaa ya wote badala ya kushindania rangi za vyama vya siasa huku akiwataka wanachama wake wasiwatukane viongozi na wafuasi wa CCM  bali wawaeleweshe wakiona hawaelewi basi wawaombee kwa madai kuwa hiyo itajenga mshikamano na umoja miongoni mwa jamii.
Aliwataka wananchi kushindana kwa kupigania rasilimali za umma zitumike kwa manufaa ya wote badala ya kushindania rangi za vyama vya siasa huku akiwataka wanachama wake wasiwatukane viongozi na wafuasi wa CCM  bali wawaeleweshe wakiona hawaelewi basi wawaombee kwa madai kuwa hiyo itajenga mshikamano na umoja miongoni mwa jamii.
Kwenye mkutano huo wananchi mbalimbali walijiunga na Chama hicho ambapo mbowe alitoa kadi kwa baadhi ya wananchama ambapo kutokana na muda wa mkutano kuwa umemalizika huku giza likizidi iliamuliwa zoezi hilo liendelee kufanywa na viongozi wa eneo hilo ili kuruhusu msafara wa kiongozi hiyo kuondoka
MBOWE akisomewa majina yawanachama wapya na mbunge wa Arusha Mjini, Lema pamoja na Katibu wa kanda ya Kaskazini, Golugwa kabla ya kuwakabidhi kadi zao
 KATIBU Kata wa TLP, Ramadhani Sama ni mmoja waliojiunga na Chadema siku hiyo
Sent from my iPhone

0 Comments:

Post a Comment