Kulikuwa na mfalme mmoja dhalimu, ambapo
fundi seremala mmoja aliapa kumuumbua ili
kulipiza kisasi cha maovu waliyofanyiwa
wazee wake na mfalme huyo. Fundi huyu
aliahidi kumshonea mfalme vazi la kimiujiza,
litakaloweza kuwatambua wachawi wote wa
nchi ile. Seremala alisema kuwa mtu yeyote
ambaye hataliona kwa macho vazi lile, basi ni
mchawi...
Ikatangazwa kuwa kuwa siku ya maadhimisho
ya kitaifa, mfalme atatoka akiwa amevaa vazi
hilo rasmi, wananchi wote wajitokeze
uwanjani kumlaki, na endapo yeyote
hataliona vazi alilovaa mfalme, basi huyo ni
mchawi ...
Kwa miezi kadhaa, fundi alionekana
akishughulika kwa bidii katika mashine yake
akishona vazi la miujiza la mfalme. Hata hivyo
kila aliyepita kwa fundi, aliona fundi akishona
"hewa" kwani hakikuonekana kitambaa wala
kitu chochote kikishonwa. Hakuna
aliyethubutu kuuliza...
Siku ya maadhimisho ikafika, seremala
akaenda kumvalisha mfalme "vazi". Wa
kwanza kushangaa alikuwa mfalme
mwenyewe, kwani aliona seremala akimjia na
mikono mitupu, ingawa ilikuwa imeinuliwa
mfano wa mtu aliyebeba kitu. Mfalme
akajiuliza "mbona silioni vazi? Kumbe na
mimi ni mchawi!" Kwa mbwembwe nyingi
seremala akaanza kulionyesha kwa majigambo
"vazi" mbele ya mfalme, huku akimuuliza
mfalme kama amelipenda. Mfalme akalisifia
vazi na kusema ni zuri na amelipenda, na
kwamba linamfaa...
Baada ya seremala kumvalisha mfalme "vazi",
mfalme akapanda farasi na kuelekea
uwanjani, ambapo maelfu ya wananchi wa
nchi ile walikuwa wakisubiri kumuona mfalme
na vazi lake la miujiza. Mfalme akatokeza. Kila
mtu aliona kwamba mfalme hajavaa nguo
yeyote. Kuanzia mfalme mwenyewe, maaskari
walinzi na hata wananchi wote. Lakini hakuna
aliyekubali kusema kuwa halioni vazi la
mfalme, maana kwa kusema hivyo, basi wewe
ni mchawi, ndio maana hulioni vazi... Watu
wakapiga makofi na vigelegele kulisifia vazi la
mfalme, ingawa kila mmoja moyoni kwake
alikuwa anajuta kuwa halioni vaxi, hivyo
pengine yeye ni mchawi! Askari nao walikuwa
makini kusikia ni nani angesema halioni vazi,
ili wamkamate mchawi...
Kwa bahati mbaya yupo mama mmoja
ambaye alikuwa ameenda na mtoto wa miaka
miwili huku amembeba mabegani, ili amuone
mfalme vizuri. Mfalme alipokaribia pale
penye mtoto, mtoto akaropoka...
"MAMAAA.... MBONA MFALME HAJAVAA
NGUO?" Mfalme akagutuka, akamwangalia
yule mtoto kwa ukali. Mtoto akaendelea
kupiga kelele huku akicheka...
"Hahahahahahaa... oneni utupu wa mfalme...
hajavaa nguo huyooo"... Kila mtu akajiuliza,
inawezekana katoto kadogo vile ni kachawi?!
Maaskari hawakuthubutu kukakamata. Baadae
watoto wengine waliokuwa uwanjani pale nao
wakadakizia... huyooo... hajavaa nguo
huyooo... Kama mzaha, umati wote
ukadakizia... "huyooo... hajavaa nguo mfalme
huyooo"... Hoja ya uchawi ikasahaulika, na
kweli hata alipojitizama tena mfalme,
akajiona hajavaa nguo... Vurugu na nguo
kuchanika, ama kweli mfalme kaumbuka...
Seremala alishatoroka zake saa hizo, na
keshafanikiwa kumuumbua mfalme...
(Hadithi hii haifundishi chochote,
inaburudisha tu)...
Hadi sasa CCM wamewatisha wabunge wao,
sio leo tu bali hata siku za nyum kuwa
atakayekuwa na msimamo kinyume na
chama, huyo ni "msaliti" na atakiona... Hadi
sasa tunaona wabunge wa CCM wakiwa
"watiifu" kwa chama, wakisifia msimamo wa
chama, kuusifu na kuukubali lakini wengi
mioyoni mwao wanajua kuwa ni msimamo
potofu. Hata hivyo nani akubali kuwa wa
kwanza kuuita "potofu"? Nani akubali
kuonekana msaliti?
Binafsi naamini kuna siku, bila kutarajia,
huku wakiamini wote "wametulizwa", CCM
wataumbuliwa na sauti ya mmoja wao
ambaye atakuwa sawa na yule mtoto wa
miaka miwili... Ataanza mmoja watakuwa
wawili, kisha watano, ishirini, mia... ghafla
mfalme ameumbuka...
VIJANA WAKUMBUSHWA KULINDA TASWIRA YA NCHI KIMATAIFA
-
Serikali imewataka vijana wanaopata fursa za ajira nje ya nchi kuwa
mabalozi wa Taifa kwa kuzingatia nidhamu, uadilifu na tamaduni katika nchi
wanazokwenda...
21 minutes ago
0 Comments:
Post a Comment