Tuwangalie kwa jicho angavu
Ni tatizo tusilolijua
Pande mbili za mheshimiwa na
tusiyoyakumbuka
Wanajamvi tutakuwa na sehemu I-III
kuhusiana na mwenyekiti wa bunge la katiba,
tukimwangalia alipotoka alipo na aendako.
Kwa mwenendo wake wengi tunajiuliza kama
keshakata tamaa na sasa anahitimisha safari
yake ya kiasiasa
Sehemu ya I
Mwenyekiti wa bunge la katiba(BMLK) Mh
Samwel Sitta ni mwanasiasa asiyeleweka kwa
wengi. Amejaliwa kipaji cha kuongea,busara
na kujenga imani kama mmoja wa Wazelondo
wa nchi hii.
Historia yake ni ndefu katika umri wa miaka
71. Sitta ni msomi wa sheria akiwa mhitimu
kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaa. Alianza
masomo yake mwaka 1964 na kumaliza
mwaka 1971.
Miaka 7 chuoni UDSM haikuwa rahisi, naye
kama walivyo wanasiasa wengine aliwahi
kufukuzwa chuo mwaka 1966 katika ule
mgomo wa kujiunga na JKT.
Mgomo huo uliitingisha nchi lakini si
mwalimu Nyerere. Wanafunzi wa chuo kikuu
walimpa mwalimu ‘ultimatum’ kuhusu madai
yao. Hatimaye wakajikuta uso kwa uso na
mwalimu na ndipo walipokabiliana na nguvu
ya hoja na nguvu za dola.
Wengine waliokuwepo ni akina Warioba na
viongozi wengine.
Samwel Sitta amelihudumia taifa katika ngazi
ya serikali na chama akiwa waziri, katibu wa
chama, mkurugurenzi mtendaji wa mashirika
ya umma n.k.
Hiyo pengine ni pamoja na kuwa na diploma
katika mambo ya utawala kulikompa nafasi
zaidi
Kwa haraka haraka Sitta anaonekana kama
miongoni mwa wanafunzi watiifu wa Nyerere.
Hata hivyo muda umetueleza bila kificho
akina nani walikuwa watiifu na wepi walikuwa
na woga wakiwa wanafunzi wanafaniki.
Sitta ilichomoza akiwa miongoni mwa wapiga
debe wakubwa wa EL katika chaguzi za
mwanzo. Tunakumbuka jinsi Mwalimu
alivyomuangalia EL kwa jicho la hofu na
uhalifu.
Pamoja na hayo sitta alikuwa mstari wa
mbele kumuunga mkono
Sitta alikwenda mbali kupingana na Nyerere
dhidi ya uteuzi wa mh EL.
Hata pale wenzake akina JK, Lukuvi, Seif
khatibu walipoonekana kunywea, Samwel
alisimama kidete na Swahiba yake EL.
Harakati zake zilifika mwisho ndani ya NEC
pale mwalimu alipomtaka Sitta kama waziri
wa sheria asome faili la EL na kuwaeleza wapi
alikuwa anaonewa.
Hapo hakuwa na ujanja bali kuahirisha
harakati zake.
Samwel Sitta ni mmoja wa wanamtandao
ambao si tu walinyanyasa watu wengine bali
pia waliwadhalilisha baadhi ya viongozi kwa
kutumia nafasi zao. Mtandao huo uliundwa ili
kuwabomoa wazee kama akina Malecela na
wengine, Sitta akiwa mshiriki.
Matarajio ya Samwel Sitta kuchukua nafasi
yalizidi pale Nyerere alipohitimisha safari ya
EL. Ikumbukwe mtandao uliendelea na
harakati hadi chaguzi zilziomwingiza JK
magogoni.
Sitta akatumia fursa hiyo kunyemelea kiti cha
uwaziri mkuu kwa vile tu EL alishachafuka na
hivyo hakuwa chaguo tena siku za mbeleni.
Katika hali isiyotarajiwa na akiongozwa na
vigogo wa mtandao wenye nazo, JK alijikuta
akimchagua EL. Jambo hilo halikuwa habari
njema kwa Sitta .
Hata hivyo Sitta akiwa mwanamtandao
akatunukiwa nafasi ya Uspika.
Zipo habari za yeye kuomba msafara kama
kiongozi mkuu.
Hilo likakataliwa ndipo nyongo na chuki
zikaanza, mtandao ukaanza kumeguka kidogo
kidogo.
Ilipotokea nafasi ya Richmond, Sitta hakusita
kuitumia vema na mzee wa Monduli akajikuta
kaangukia pua.
Sehemu itaendelea..........
Richmond na viporo alivyofunika
Posho za wabunge na alivyowageuka
wananchi
n.k
Sehemu ya II
SITTA NA HISTORIA YA TANGANYIKA
Kabla hatujarudi bungeni alipokuwa Spika na
sakata maarufu la Richmond, tungependa
kuwakumbusha kuwa majuzi alipokuwa
anawania nafasi ya uenyekiti, Sitta alisema
yeye ni chura anarudi majini. Wengi
hawakuelewa maana ya kauli hii. Hapa Sitta
hakumaanisha kuwa alikuwa Spika anarudi
kuwa Spika. Maana yake ina uhusiano na
Tanganyika
Tumeeleza jinsi alivyokuwa sehemu ya
Mtandao wa JK. Lakini si mara yake ya
kwanza, Sitta alipokuwa waziri wa sheria na
katiba lilikuwepo sakata la G55.
Tunachofahamu Sitta aliunga mkono kundi la
G55 japo alikuwa waziri. Yupo katika kumbu
kumbu akieleza maandalizi yalikuwepo kuwa
na kura ya maoni(referendum) baada ya hoja
za G55 kugonga mwamba kiufundi(On tech
ground)
Katika bajeti ya wizara yake, mh Sitta aligusia
suala hilo la kuwa na kura ya maoni (1995?).
Kilichomfanya asijitokeze wazi katika nafasi
ya G55 ni nafasi yake ya uwaziri.
Hivyo anaposema chura anarudi majini ni
wazi anajua kuwa ni suala la Tanganyika
lanalolifahamu siku nyingi tu.
Kama ilivyokuwa huko nyuma, akiwa waziri
wa sheria mh alishindwa kusimamia suala la
kurudi kwa Tanganyika.
Uzalendo wake ukaishia katika chama zaidi ya
imani yake juu ya uwepo wa Tanganyika.
Hivyo ni vema kabisa kusema suala la
muungano loyality ya Sitta ni uwepo wa
Tanganyika.
Tatizo ni kuwa, Sitta amefungwa na uchama
zaidi ya uananchi.
Akiwa Spika wa bunge 2005-2010 mara
nyingi amesikika akitoa kauli tata. Kwa
mfano, ni sitta aliuliwauliza wznz kuhusu
gharama za elimu ya juu n.k
Lakini ni Sitta huyo huyo alisema ni haki kwa
wazanzibar kuwazuia Watanganyika kupata
ardhi kwasababu kuna eneo kubwa
Tanganyika. Kwamba Tanganyika kuwa na
eneo ni shamba la bibi na muungano uliopo
ni safi kabisa.
Misimamo ya Sitta inakuwa ya pande mbili na
ni ngumu kuelewa anasimamia wapi.
Ni mtu anyejificha nyuma ya agenda na
kuchagua upande baada ya kuona uelekeo.
Katika bunge la katiba Sitta amesikika akitetea
kura ya siri lakini akichagiza kura ya uwazi.
Naye ni mtu anayependa kuchagua upande
kutokana na mwelekeo na wala si maoni au
maono yake binafasi.
Kwasasa hivi anaonekana kuwa ni muumini
wa muungano wa serikali 2, kinachomsukuma
zaidi ni nia yake ya kuwania Urais 2015. Sitta
anafahamu kuwaudhi wahafidhina wa CCM ni
kujitafutia madhara. Hilo alilionja wakati wa
sakata la Richmond.
Sakata la Richmond lilitokana na hasira zake
dhidi ya Mtandao uliomtupa na kumpa nafasi
ya Spika.
Tunakumbuka iliwahi kutokea viongozi wengi
walikuwa nje ya nchi na Spika akakaimu
nafasi ya Urais na kupewa piki piki za
kumsindikiza. Zote hizo zilikuwa ni jitihada za
kumpooza. Na kila mara kiongozi mkuu wa
serikali anapokuwa hayupo bungeni nafasi
hiyo hupewa kwa vile ni sehemu ya mtandao.
Sakata la Richmond nalo halimuachi kama
alivyo. Mara ya kwanza aliafiki kuwa
hakukuwa na hujuma hadi kamati ndogo ya
shelukindo iliposema kuna umuhimu wa
kuchunguza zaidi.
Kwavile kamati ile ilikuwa ya bunge ikiwa na
CCM wengi, mh alikubali. Nafasi ya
kumfanyizia mh E ilipotimu akaitumia vema.
Kitu wengi wetu tusichokumbuka ni kuwa
sakata lile halikuisha na ukweli wake
ulifichwa.
Hata pale walipojitokeza watu kutaka kueleza
ukweli na undani wake Spika Sitta alizima
hoja hiyo.
Ndivyo alivyozima hoja za Meremeta na
zinginezo kwa kigezo cha 'kiti' kimeamua
Kilichomsukuma kuzima hoja hizo ni ukweli
kuwa bado alikuwa na matarajio ya Uspika na
pengine nafasi ya juu zaidi.
Hata hivyo wahafidhina hawakumuacha,
ndani ya CC uteuzi wake wa Uspika
ukahitimishwa kwa sababu rahisi, ni zamu ya
akina mama.
Hilo lilikuwa pigo kubwa kwa Sitta ambaye
alikuwa anataraji kujenga mazingira ya Urais
kupitia simple popularity kama Richmond.
Ukweli unabaki kuwa Richmond na undani
wake ulifichwa na kuzikwa na Sitta.
Ni kutokana na kutomwelewa, wengi waliona
anafaa kuwa mwenyekiti wa bunge la katiba.
Sitta anatumia nafasi hiyo si kwa sababu ya
kuipenda nchi yake, ni kutafuta umaarufu wa
kujenga jukwaa (Platform) kwa ajili ya 2015.
Ni kwa msingi huo tulishawahi kuonya
mapema kuwa huyu si mtu wa kuaminika.
Anajali masilahi yake kuliko ya nchi, na ni
mwepesi sana wa kuitumia nchi kufikia
malengo yake.
Ingawa sasa hivi anaonekana kuwa CCM, Sitta
ni muumini mzuri wa Tanganyika kutokana na
historia yake. Kinachomsukuma ajali CCM
katika mchakato ni ukweli kuwa
alishawahi'kuumwa na nyoka' wakati wa
kugombea Uspika.
Anafahamu kuwaudhi CCM kutahitimisha
mbio zake haraka iwezekanavyo.
Ili kuwafurahisha CCM kwa kujenga mazingira
ya baadaye na si ya nchi, Sitta amechukua
uenyekiti na kwenda kinyume cha kanuni
zilizoandikwa. Aliamua kumwita Warioba
kwanza kabla ya JK ili kutoa nafasi ya
kumbomoa, kumdhalilisha na kumfehdehesha
jambo alilofanikiwa. Hakufanya hivyo kwa
kukurupuka anafahamu umuhimu wa CCM na
umhimu wa kutetea mtandao ambao
anategemea utamwezesha kuelekea 2015.
Hatua ya pili ilikuwa kuwatisha wale
wanaopinga muungano wa serikali 2.
Sitta amenukuliwa akisema atapamaba na
wote wanaopinga muungano.
Hapa alimaanisha wanaopinga serikali 2 si
kwasababu anaamini serikali 2 bali anataka
kuwafurahisha CCM kwa gharama za
mamilioni ya Watanganyika wanaodai serikali
yao.
Hatua ya tatu ni kuunda kamati
zitakazosukuma agenda ya serikali 2 kwa
nguvu.
Kamati hizo zimesheheni na kupangwa CCM
kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Hilo ndilo alilotaka kwavile anaamini kupitia
katib atakuwa amefungua milango ya
kuelekea 2015.
Safari ya 2015 ameshainza, ingawa wengi
hawafahamu, naye kama EL ametumia
sehemu kama makanisa kuhakikisha anajiweka
sawa. Hivyo kuunga mkono CCM kwa nguvu
zote ni kuimarisha harakati zake hata kama
kufanya hivyo ni kwa hasara ya nchi.
Je, move anayoifanya itamsaidia au
itahitimisha safari yake mapema sana?
Bunge hili litamvumilia au litamvunjikia
mikononi?
Sehemu ya III
UNDUMILA KUWILI WA SITTA NI WA SIKU
NYINGI
Wakati bunge linazinduliwa Spika Sitta akiwa
katika kiti, jambo la kwanza lilikuwa
kumwalika rais azindue.Hilo ni baada ya
Wabunge kuapishwa. Ndio utaratibu
umetumika miaka nenda rudi.
Ni nafasi ya Rais kueleza vipaumbele vya
serikali yake.
Bunge maalumu la katiba linaloendelea
liliandaa utaratibu kama huo tofauti ikiwa ni
Rais kuzungumzia mambo ya kitaifa
yanayohusiana na katiba.
Katika hali tuliotarajia wengine na tuliyowahi
kuieleza Spika Sitta akaamua binafsi kwa
kutumia 'busara zake' kumwalika Warioba
kwanza ili Rais afuatie.
Busara anazozisema Sitta ni kuwa bunge
lazima liwe na agenda kwanza ili Rais aje
kulihutubia.
Licha ya wanasheria kuandaa kanuni hizo
wakiwemo wenye busara zaidi, Sitta akatumia
nguvu na ubabe wake kuhakikisha mkakati wa
kuwadhalilisha wazee wenzake akina Salim
Ahmed Salim, Jaji Warioba,Jaji Augustino
Ramadhan, marofesa na madaktari unatimia
kwa kupindisha kanuni.
Hilo amefanikiwa na JK kamvuruga mzee
Warioba kama mtoto mdogo kwa kumzushia,
kumzogoa na kumnyanyasa hata kwa
asichokisema. Azma ya JK kupitia Samwel
Sitta ikatimia.
Ni ngumu kuamini dhalili aliyopata mzee
Warioba, alipaswa kupewa makamu wa Rais
na waziri mkuu wa zamani. Samwel Sitta
akaona ni bora amdhalilishe mzee mwenzake
ili kufungua njia kuelekea 2015. Sijui kama
mkakati huo utamsaidia maana historia ni
mwalimu mzuri sana.
Huo ni undumila kuwili kwasababu alipokuwa
anajinadi alisema anakwenda kutetea taifa na
kwamba Tanzania kwanza.
Kinyume chake Tanzania pili, Sitta kwanza na
CCM muhimu.
Ni undumila kuwili wa namna hiyo uliwahi
kujitokeza katika bunge alililoongoza huko
nyuma.
Baada ya wazee wa Dar es salaam kulalamikia
posho na marupu rupu aliyoandaa Sitta, Rais
alikubaliana nao hadharani.
Nyuma ya pazia Samwel Sitta akamshawishi
rais kuhusu posho hizo na zikaongezwa
kinyemela.
Hata alipoulizwa, Sitta alisema mshahara wa
mbunge ni siri. Huyu mtu anayeitetea
Tanzania hawezi kujadili mshahara wa
mbunge ni mtetezi gani huyu.
Huyu ndiye anayepita makanisani na
mashuleni akisema anapinga ufisadi na watu
wanamwamwini. Ni jambo la kushangaza sana
kwasababu Samwel Sitta ndiye aliyezika hoja
ya pesa za radar isijadiliwe bungeni kwa
nguvu za kiti cha Uspika.
Leo tunaaminishwaje kuwa Samwel anapiga
vita ufisadi?
Kila kiporo cha tuhuma kisicho na majibu,
Sitta ameshiriki kuficha.
Tunakumbuka matumizi mabaya ya fedha za
ofisi. Leo tunaambiwa ni mwadilifu
Jana amesikika akisema uchaguzi wa wenyeviti
hana lawama kwasababu CCM ni wengi na
hata katika kura watashinda. Huyu ndiye mtu
aliyeomba kiti kwa kauli mbiu ya Tanzania
kwanza.
Leo hawezi kuliangalia bunge kama Tanzania
bali CCM halafu tunaaminishwa ni mtu safi.
Anaongea jambo moja leo kesho anabadilika
na msimamo tofauti.
Katika bunge aliloongoza kabla kama Spika,
wenyeviti wa kamati za bunge baadhi hutoka
vyama vya upinzani kwa kanuni ili kuleta sura
ya bunge.
Mbona alipokuwa Spika hakuwahi kusema
CCM ni wengi na hivyo waongoze kamati?
Huu kama si unafiki na undumila kuwili ni
kitu gani wanajamvi?
Anachoshindwa kukielewa Sitta ni kuwa
katiba ni agenda ya wananchi bila kujali
CCM.Chadema/CUF au TLP. Mbinu
anazotumia si kuwa zinawadhalilisha
wananchi bali zinamweka mahali pagumu
sana kiheshima,nafasi katika jamii, umri na
matarajio ya baadaye.
0 Comments:
Post a Comment