SOMA SURA YA KWANZA.
SEHEMU YA KWANZA JAMHURI YA MUUNGANO NA WATU.
No2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
Mshangao kimsingi unakuja hapa, hv unapo ulizwa Tanzania ni nini na baada ya kujibu ni nchi iliyo mashariki mwa bara la afrika, nadhani ufafanuzi utakao endelea nao ilikumtambulsha anayetaka kujua nini Tanzania utamwambia ni Jina la taifa lililotokana na Muungano wa mataifa mawili ya Tanganyika na Zanzibar hapa utakuwa umeeleweka na mwenye akili timamu.
Upotoshaji tena wa makusudi ktk katiba hiyo ni pale katiba ilipotamka hivi 1.Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano. hapa walikuwa sahii kwani kitu 1kinapounganka na kingne kimoja au zaidi matokeo yake huitika kwa jina la umoja.
2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar nakomea hapa.
Ufafanuzi.
Hapa unaweza ukajiuliza na usipate majibu ukiwa huna akili sawa sawa ingawa kwa ujuha unaweza ukajiridhsha kuwa umewaelewa watunzi wa katiba hii mamemaanisha nini kusudi na lengo lao pia ni nini.
Wenye akili haya ndyo maswali yao, Ikiwa katiba ya mwaka 1977 inautambua Muungano huu kama ni wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar Je ule Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Taifa la la pamoja linaitwaje? Je Kama Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na Zanzibar mwaka 1964 je Tanzania bara na Tanzania Zanzibas zilipata uhuru mwaka gan na Walitawaliwa na taifa gani?
Mimi NNKUMBUKILA ni mtoto wa mzee MILANZI, mke wangu SOMOE ni mtoto wa mzee HOKORORO ndoa yetu haiwezi kubadili uasili au ubn wa yeyote kati yetu ingawa ktk ulmwengu wa kisasa ktk utambulsho wa pamoja familia yangu itatambulishwa kwa jina la mr and mrs NNIKUMBUKILA lakini unapotaka kujua waliounga familia hii mimi nitajitaja kwa jina langu kamili yaani NNIKUMBUKILA MILANZI, na mke wangu SOMOE HOKORORO.
MASWALI KWA KATIBA YA 1977.
Upotoshaji wa majina ya nchi zilizoungana ulfanywa kwa bahati mbaya au ni makusudi?
Kama ni bahati mbaya mbona kuna marekebsho mengi sana ya katiba hii mpaka toleo la mwisho la mwaka 2005 bado hawajaondoa makosa hayo?
Kama ni makusudi ni kilikusudiwa nini?
Kupotosha vizazi hv vya shule za kata kutokujua asili yao? Kulifuta taifa la tanganyika na baade Zanzibar? Je yote haya ni kwa maslai ya nani na ili kiwe nini?
Majibu yapo wazi ndyo maana mpaka leo kwa kuwa walioshiriki kwa namna mmoja ama nyngne kuandika katiba hii ya mwaka 1977 na marekebisho yake bado wapo wakiongozwa na nguvu za kinsyuka mzimu wao wanabaki na msimao wao wa 2, 2, 2 kuelekea 1 hapa ndyo lengo lao.
Lakni wanapaswa kufahamu kuwa asili huwa haipotei Tanzania itapaki kuwa ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na si kinyume cha hapo.
Ileweke kuwa MZEE KARUME mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi alikuwa ni Rais wa Zanzibar kabla ya Muungano si Tanzania Zanzibar na Julius Nyerere mwenyezi mungu amlipe anavyostaili alikuwa Rais wa Tanganyika na si Tanzania Bara, na baada ya Muungano MZEE KARUME Mwenyezi mungu amjaalie pepo ya daraja ya juu alikuwa ni RAIS wa Zanzibar na makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Julius Nyerere mwenyezi mungu amlipe anavyostaili kulipwa alikuwa ni Rais wa Tanganyika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini baada tu ya Muungano huo Tanganyika ikapotezwa kimya kmya na kwa kulithibtsha hlo mpaka ktk vtabu vyao wakahakksha neno Tanganyika linafutwa na ndyo maana ata katiba hii ya mwaka 1977 imejaa upotoshaji mkubwa.
HUU NI MSAADA KWENU VIJANA WENZANGU WA LEO TOKA KWA KIJANA MWENZENU WA ZAMANI YERICKO NYERERE, AHSANTENI.
TUNAITAKA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZENYE MAMLAKA KAMILI
0 Comments:
Post a Comment