Wabunge wa CCM ambao wanahudhuria mkutano wa Bunge maalum
la Katiba wameingia katika mgogoro na mzozo mkali wenyewe kwa wenyewe
na kuamua hata kususa kuhudhuria vikao vya kichama (party caucus) kwa
ajili ya kuweka misimamo.
Chanzo cha mkwaruzano wa wabunge hao ni kitendo cha vigogo wa chama
hicho kuwateua Ole Sendeka, Peter Serukamba na Ummy Mwalimu kuwa ndio
pekee watakuwa wakiwakilisha maoni na misimamo ya chama katika kipindi
chote walichokuwa wakijadili rasimu ya kanuni za bunge hilo. Wale
waliokuwa wakifuatilia bunge watakuwa wanalikumbuka swala hilo vema.
Hali hiyo imewafanya wabunge wengine wa CCM kuona kuwa wamepuuzwa na
chama huku watatu hao wakitafutiwwa umaarufu wa nguvu kupitia kanuni
hizo huku mambo mengi waliyoyaombea marekebisho yakitoka kwa Andrew
Chenge na kuzungumzwa na watatu hao pekee.
Aidha watatu hao waliamua kula dili pia na mtumishi mmoja wa Bunge
aliyetoka Baraza la wawakilishi Zanzibar kupenyeza majedwali ya
mabadiliko kwa Mwenyekiti Kificho kabla ya Waziri wa sheria zanzibar
ambaye ni mjumbe wa Kamati wa kamati ya kanuni kustukia dili hilo na
kumwambia mwenyekiti kuwa baadhi ya mapendekezo yanayotolewa na akina
Ole sendeka na Ummy hayakuletwa kwa wakati lakini yamepenyezwa kijanja.
Uchunguzi ulifanyika na kubainika kuwa mtumishi huyo ndie aliyekuwa
akitumiwa na akina Ole Sendeka na sasa mtumishi huyo amerejeshwa kwao
Zanzibar.
CCM kwa sasa hawahudhurii kikamilifu vikao vya kichama na kuwaachia
wabunge wachache na mfano mzuri ni kikao cha juzi ambacho kilihudhuriwa
na wabunge wasiozidi 100 wa CCM huku wengine wakiweka mikakati yao
binafsi ya kupinga mwenendo wa wenzao katika mkutano huu.
Hata swala la Kura ya siri au wazi ambalo limeachwa pending na kanuni,
lilishindwa kufikiwa muafaka kwa sababu ya wanaCCM wengi kususia
mikutano na kuwaacha Ole Sendeka na wenzake wakishikia bango kwa niaba
ya chama na sasa wanategemea Rais JK ataukata mzizi wa fitna atakapokuja
kuzindua bunge Ijumaa au Jumamosi wiki hii kwa kuzungumzia msimamo wake
kuhusu aina ya kura na huo ndio unatarajia kuwa msimamo wa bunge pia
hapo mbele ya safari.
DKT JINGU AWATAKA WAKUU WA VITENGO VYA HABARI SERIKALINI KUTUMIA MAJUKWAA
YAO KUELIMISHA JAMII KUHUSU KAZI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI
-
Na Mwandishi wetu Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi
Maalum, Dkt. John Jingu, amewataka Wakuu wa Vitengo vya...
37 minutes ago
0 Comments:
Post a Comment