Katika kukabiliana na vitendo vya
ujangili vinavyoendelea kushika kasi ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu,
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) litaendeshwa katika mfumo wa jeshi-usu
katika siku chache zijazo ambapo watumishi wake watalazimika kupitia katika
mafunzo maalum ya kijeshi.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA aliyasema
hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifunga rasmi mafunzo ya askari wapya 96
walioajiriwa na TANAPA na kuhudhuria mafunzo ya miezi minne katika Hifadhi ya
Taifa Katavi mwishoni mwa wiki.
Kijazi alisema kuwa TANAPA imeanzisha
utaratibu mpya ambapo sasa askari wanaoajiriwa na shirika kutoka katika Vyuo
vya Wanyamapori vya Mweka na Pasiansi pamoja na wale wa kutoka Jeshi la Kujenga
Taifa watalazimika kupitia mafunzo maalum yanayoandaliwa na shirika kwa ajili
ya kuwawezesha waajiriwa wapya kufahamu mazingira halisi ya utendaji kazi
katika eneo la uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi za Taifa.
Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo
Sajini Taji Simon Mbunda akipokea zawadi yake iliyotolewa na wahitimu
kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Katavi Ignas Gara akiongea wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo.



0 Comments:
Post a Comment