KARIBUNI TENA WASOMAJI WANGU



Wasomaji wangu wapenzi kwanza niwaombe radhi kwa kutowapa taarifa mpya kwa takribani zaidi ya mwaka mmoja


Ninaowamba mnisamehe kwani pengine sababu zilizopelekea hayo zinaweza zisipokewe kwa uzito sawa miongoni mwenu.


Kama mnavyoona niliweka taarifa ya mwisho October 13, kwa bahati mbaya  alifajiri ya October 14, 2012  siku ya jumapili majira ya saa 11:40 dada yangu mpenzi rafiki yangu wa karibu swahiba wangu na msiri wangu mkuu Vicky Bahati aliondoka katika ulimwengu huu na kurudi kwa baba yetu wa mbinguni.




Kuondoka kwa rafiki yangu huyu ilikuwa ni jambo gumu ambalo kwanza lilinishtusha sikutegemea kama anaweza kuondoka ghafla hivyo niliumia sana kwani nilitamani ningekuwa karibu yake nimsaidie.

Niliumia kwa mambo mengi wakati mwingine nikijilaumu kwa nini sikufanya jitihada nifike Iringa pengine ningeweza kumzuia  Yule nesi wa hospitali ya mkoa wa Iringa ambaye alimchoma sindano ya usingizi asifanye hivyo.


Nesi huyo ambaye nilipigiwa simu na mdogo wangu Charles na shemeji yangu Philemon wakiniambia wanamuuliza anamchomaje sindano Vicky kwa maelekezo ya simu anayopewa na dr lakini hakutaka kujibu zaidi ya kuendelea na zoezi lake la kuchoma sindano.

Inaniuma kwani nilitamani ningekuwepo kwani ningeweza hata kuisoma dawa anayomchoma lakini sikuwa na uwezo wa kusafiri kwa wakati huo kwani nilikuwa mjamzito na safari ya Arusha mpaka Iringa dr alinishauri si sahihi kiafya.



Iliniuma na inaendelea kuniuma kwani baada ya kuchomwa sindano hiyo waliniambia Vicky ambaye alikuwa akisumbuliwa na malaria na ilikuwa inamfanya anapoteza kumbukumbu anaongea mambo yasiyoeleweka alilala usingizi.



Lakini baada ya nusu saa nikapigiwa simu tena nikiambiwa niendelee kumuombea kwani anakoroma sana nikawaambia wamweke shingo vizuri nikawaambia wajaribu kumwangalia dr wa zamu ili aweze kumhudumia zaidi lakini jibu likawa hakuna dr ni nesi ni yuleyule ambaye hataki kutoa majibu ya maswali anayoulizwa kuhusu afya ya mgonjwa.



Kwa keli sikulala nilikuwa nikiendelea kuongea na Mungu wa mbinguni amponye dada yetu huyo kwani sisi tuko watatu tu kwa mama yetu mpenzi Cecy ukimchukua tutaumia sana, nilikuwa najua Vicky ni mpiganaji jasiri si legelege hajawahi kulazwa hospital toka amezaliwa kwa hiyo nikazidi kumlilia Mungu kwa kuwa hii ni mara ya kwanza kuumwa hoi amponye ili apate kuyasimulia matendo yake makuu.



Lakini Mungu alikuwa na mipango dhidi ya Vicky Saa 11.39 asubuhi Charles ananipigia simu akilia ananiambia Vicky ameondoka sikuamini nililia sana lakini akili yangu ikafanya kazi mara moja mama yangu ni mgonjwa wa sukari nahitaji kuwa jasiri ili nimnusuru na madhara ambayo yanaweza kupelekea na yeye kupoteza uhai.




Nilikuwa nyumbani na wafanyakazi na mtoto wangu wa 4 yrs  Albert Mume wangu alikuwa amesafiri nilimsikia  Vicky ananiambia “umeshakuwa sasa simama uhakikishe kila kitu kinakuwa sawa ukweli ni huo na hakuna wa kuubadilisha” na kweli kwa uwezo wa Mungu niliweza.



Ila mpaka sasa bado naamini rafiki yangu yuko salama kwa baba, na naamini kila jambo ni mpango wa Mungu hayo yaliyotokea Mungu ameyakubali kama asingeyakubali yasingetokea.





“Ila rafiki yangu Vicky hakuna aliyeweza kuvaa viatu vyako kila mmoja anahisi kupungukiwa wewe ni mama bora kwa Brightness na Bakili hakuna atayeweza kuchukua nafasi yako”.




Wakati tunaipamba nyumba yake ya milele nilijiuliza hivi haya yanaweza kubadilisha ukweli kuwa ameondoka nikajijibu ukweli huo haubadiliki lakini kwa tabia yake alipenda kutengeneza vitu vyake vya muonekano tofauti basi na nyumba yake aliyopumzika tukaifanya ya kivyekovyake kama ulivyozoea kuniambia.

“Vicky sina mtu ambaye naweza kuongea naye na simu kila saa, kuchat naye kwa msg kama vile wala wa kuweleza huzuni, raha karaha navyokumbana navyo, japo nimejaribu kumweleza dr kuwa bado mimic na wewe huwa tunaongea amenikatalia ananiambia ni mawazo yangu ila mimi naamini ni wewe dada japo nilikuwa nikikuita dada unashtuka kuwa nataka kukuomba nini leo pia nakuita dada nikiamini utacheka kama kawaida yako”

Kwa kifupi hiyo ndiyo ilifanya mkakosa mambo mapya kutoka kwangu naomba wale ambao hawaoni umuhimu wa niliyoyaeleza samahani na wale ambao hawakupenda mniwie radhi na wale walioguswa poleni ila tukimtumainia Mungu yote yawezekana.


SAFARI YA MWISHO YA MPIGANAJI VICKY MACHA LEO NYUMBANI KWAO MOSHI


Mwili wa marehemu Vicky Macha ukisaliwa ndani ya eneo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya KCMC.
Msafara kuelekea Rau mjini Moshi nyumbani kwa mume wa marehemu.
Mama wa marehemu akiaga...
Grace Macha, mdogo wa marehemu akiaga mwili.
Mtoto wa kwanza wa marehemu
Mtoto wa pili wa marehemu (picha na Mjengwa Blog)


0 Comments:

Post a Comment