KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha, Mary Chatanda alijikuta katika wakati mgumu kutokana na kuzomewa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Uchaguzi wa mkoa uliofanyika Oktoba 11, mwaka huu baada ya kutambulisha viongozi waliokuwa wamekaa meza kuu huku akimruka mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.
Hali hiyo hiyo imetafsiriwa tofauti na baadhi ya wajumbe wengine wakidai kuwa ni tukio la bahati mbaya lakini wengi wao wakidai kuwa limesababishwa na katibu huyo kuona kundi analolinunga mkono limeangushwa vibaya kwenye chaguzi zinazoendelea huku kundi la Waziri Mkuu huyo mstaafu liibuka kidedea.
Makundi hayo yametokana na mbio za kuwania kuteuliwa kugombea Urais kupitia CCM 2015 ambapo juzi Chatanda alinusurika kupigwa wakati alipokuwa akisimamia uchaguzi wa Mwenyekiti wa UV CCM mkoa baada ya kujaribu kujenga mazingira ya kumwezesha mgombea aliyekuwa akimtaka,Dk Harold Adamson kuibuka mshindi jambo ambalo halikufanikiwa kwani aliyeibuka mshindi ni Robinson Meitenyiku.
Jana Chatanda ambaye alikuwa msimamizi msaidizi alizomewa wakati alipokuwa akitambulisha viongozi waliokuwa meza kuu wakati wa mkutano huo uliwashirikisha wajumbe 855 ambao ulifanyika kwenye kwenye Hoteli ya Naura Spring, ambapo Msimamizi Mkuu alikuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Jumanne Maghembe huku Lowassa akichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa muda.
hatua hiyo ya Chatanda ilipelekea wajumbe wa mkutano huo kuanza kumzomea huku wakipaza sauti wakitaka Lowassa atambulishwe hali iliyomlazimu Katibu huyo wa mkoa kuomba msamaha na kumtambulisha Lowassa akasimama na kupunga mkono ndipo ukumbi wote ukalipuka kwa shangwe huku wakiimba “CCM, CCM, CCM” na wengine wakipiga vigelegele na shangwe za kimasai.
Akifungua mkutano huo Waziri Maghembe aliwataka wajumbe kuacha kuzomea au kushangilia wagombea wanaowataka au wasiowataka pindi watakapofika mbele yao kwa ajili ya kjuomba kura ili kuwezesha uchaguzi huo kumalizika kwa amani.
Alisema kuwa lengo la uchaguzi huo ni kupataviongozi watakaojenga chama kwa kuhakikisha wanavunja makundi na kuwaunganisha wanachama wote ili kuhakikisha viti vya Udiwani na Ubunge vilivyopotea vinarudi CCM.
“Msichague Viongozi watakaobweteka na kutugawa, hawa hawatufai,
tuepuke viongozi wa aina hii, tuchaguwe kiongozi atakaye
Prof Maghembe alisema kuwa amelazimika kuomba ulinzi wa kutosha toka kwa Mkuu wa Mkoa Arusha, Magesa Mulongo, ambaye naye ni mjumbe wa mkutano huo ambapo amempatia Polisi wa kutosha ambao alidai kuwa wapo kwenye eneo hilo wakiwa na sare na wengine wakiwa wamevaa kiraia.
Akiongea kwenye mkutano huo mara baada ya wajumbe kumchagua kuwa Mwenyekiti wa muda aliwashukuru wajumbe wote kwa kuwa na imani naye jambo liloamsha shamrashamra za kumshangilia kwa kishindo.
“Wajumbe nimewaelewa na sitawaangusha, nimewaelewa ndugu zangu
sitawaangusha, nawashukuru kwa kunishangilia, ila sasa tusishangilie
tusije kuharibu utaratibu,”alisema Lowasa.
Wagombea wa nafasi ya uenyekiti walikuwa watatu ambao ni pamoja na Onesmo
Nangole anayetetea nafasi yake, Dk. Salash Toure na Adamu Chora ambapo Nangole aliwaomba wamchague ili aweze kusimamia dosari zilizopo na kushughulika na watu wote wanaoleta makundi ndani ya chama kwa I mgawanyiko uko kuanzia kwenye wilaya mpaka mkoani.
Hata hivyo mjumbe mmoja alimuuliza kuwa atawezaje kuwarejeshea amani waliyokuwa nayo kama chama tawala kwa kuvaa nguo za kijani na kutembea kwa uhuru Arusha kwani kwa sasa hawana amani ambapo Nangole alisema kuwa ataliwasilisha kwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa, Mulongo.
Kwa upande wake Dk.Toure akijinadi alisema akichaguliwa atamaliza makundi
yaliopo ambayo yamekiathiri chama hicho tawala kwani wanachama wamegawanyika kila ngazi na kuwaomba kuwabwaga waliotumia fedha kuomba kura kwenye uchaguzi huo.
Naye Chora, aliwaomba wajumbe hao wamchague kwani ili amalize makundi yanayoangamiza chama hicho ambayo yamepelekea wapoteze baadhi ya majimbo ambapo mkutano huo uotarajiwa kuchagua wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa, Katibu wa Siasa na uenezi mkoa na Katibu wa Uchumi na Fedha.
0 Comments:
Post a Comment