UZINDUZI PREMIER PALACE HOTEL ARUSHA

MKURUGENZI WA HOTEL, ALEX MARIWA AKIONGEA WAKATI WA UZINDUZI WAFANYABIASHARA jijini Arusha wametakiwa kuacha mashindano na badala yake washirikiane katika kuhakikisha wanaongeza ajira na kukuza uchumi.

 Hayo yalisemwa juzi na mkurugenzi wa hoteli ya kitalii ya Premier Palace, Alex Mariwa alipokuwa akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa hoteli hiyo iliyopo Makao Mapya kata ya levelosi.

 Alisema kuwa watajitahidi kuhakikisha kuwa mahitaji ya vitu mbalimbali vinavyohitajika kwenye hoteli hiyo vinanunuliwa Arusha na vitongoji vyake ili kuweza kuongeza kipato cha wananchi na kujenga mahusiano mema.

 “Tupo hapa Arusha si kwa mashindano ila kufanya kazi pamoja na wenzetu wenye mahoteli na Tour Operators (mawakala wa utalii) kwa manufaa yetu wote kwa nia ya kuongeza soko la ajira na kukuza uchumi wa Taifa letu” alisema Mariwa. 



Naye Mkurugenzi Mtendaji wa hoteli hiyo, Edward Mariwa alisema kuwa waliharakisha kukamilisha ujenzi wa hoteli hiyo ikiwa ni kuitikia wito wa serikali wa kuwataka kuongeza nyumba za kulala wageni hasa kipindi hiki kunapofanyika mkutano mkubwa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaoanza leo(jumatatu).

Alisema kuwa hoteli hiyo ya ghorofa sita yenye vyumba 40 vya kulala , kumbi mbili za mikutano, baa, mghahawa na kituo cha biashara ilianza kujengwa mwishoni mwa mwaka 2009 ambapo imegharimu shilingi bilioni 1 na imeanza kwa kuajiri watu 35 idadi inayotarajiwa kuongezeka kulingana na mahitaji. 


Kwa upande wake Askofu Msaidizi jimbo Kuu la Arusha, Simon Tengesi aliyeendesha ibada kabla ya ufunguzi wa hoteli hiyo wapongeza kwa kukumbuka kumshukuru Mungu kwa kuwafanikisha kutimiza malengo yao kwani ni wengi huwa wanakumbuka kumuomba lakini wakifanikiwa hawakumbuki kumshukuru.

0 Comments:

Post a Comment