EABC Calls for Adoption of Regional Track and Trace System to Streamline Cross-Border Trade, Combat Illicit Trade, Improve Health, and Boost Government Revenue Collection

Officiating the Regional Workshop on Track and Trace Systems within the East African Community (EAC) framework, organized by the East African Business Council (EABC), Chief Guest  Exaud S. Kigahe, Deputy Minister for Industries and Trade, United Republic of Tanzania, highlighted the significant economic losses due to illicit trade, which accounts for approximately 3.3 percent of global trade according to a World Customs Organization (WCO) report.





Kigahe praised EABC and EAC for addressing illicit trade through discussions on Track and Trace (T&T) systems. He emphasized the importance of adopting a common regional and interoperable T&T solution to facilitate cross-border data sharing and cooperation, enhancing efforts to combat illicit trade within the EAC.






John Bosco Kalisa, during his remarks, noted the implementation of digital tax stamps and electronic cargo tracking systems in the EAC. He stressed that these technologies primarily focus on authentication and tax verification rather than comprehensive tracking and tracing. 

Kalisa urged the adoption of a regional T&T system to streamline trade, combat illicit activities, improve health outcomes, and boost government revenue collection. He also called for reduced costs of Digital Tax Stamps (DTS) across EAC states, highlighting the need for a regional system review.


Stellah Nyambeki Onyancha, Deputy Registrar at the East African Community Competition Authority, underscored the challenges posed by illicit trade, anti-competitive practices, and consumer violations. She advocated for collective efforts from governments, businesses, and consumers to address these issues and promote fair competition within the EAC.


Eng. Ahmad Abdeldayem Aljawawdeh, during the panel discussion on “Benefits of Digitization: Win-Win for All,” shared that Jordan experienced a 30% reduction in illicit trading and a 50% increase in production following the adoption of a T&T system. Cobus de Hart from Oxford Economics Africa emphasized that a regional T&T system would enable resource pooling, technical asset sharing, cost minimization, and improved law enforcement intelligence.



The workshop, attended by over 85 government officials, private sector stakeholders, international experts, and industry leaders, facilitated the exchange of insights and best practices. The participants aimed to develop proposals and a roadmap towards a digital regional track and trace system, a crucial tool for enhanced revenue collection and the fight against illicit trade.









 SKIMU ZA NDUNGU,KIHURIO YAJAYO NI FURAHA TUU...


Na Gift Mongi


Same


WAKULIMA zaidi ya elfu tatu katika skimu za umwagiliaji Ndingu na Kihurio katika Jimbo la Same mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro wataenda kunufaika na kilimo baada ya serikali kutoa Bilioni 7 kwa ajili ya kukarabati skimu hizo. 


Hatua hiyo imekuja baada ya mvua zilizonyesha na kupelekea kuharibu miundombinu ya skimu hizo ambazo zinategemewa kwa kiasi kikubwa kuilisha wilaya ya Same. 



Akitambulisha wakandarasi watakaojenga skimu hizo ambazo ni kampuni ya Hamieri (T) Ltd na Ansil (T) Ltd, Mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni alisema kuwa lengo la serikali chini ya Rais Dkt. Sami Suluhu ni kuhakikisha wananchi wananufaika na kujikomboa katika umaskini. 



Alisema kuwa, ukarabati wa skimu hizo unatarajiwa kukamilika baada ya mwaka mmoja na nusu na kuwataka wakandari kuhakikisha wanatoa ajira zisizohitaji utaalam kwa vijana wazawa ili waweze kunufaika na mradi huo

 RC MAKONDA AMUOMBA RAIS MWINYI KUIUNGANISHA ARUSHA NA ZANZIBAR KIUTALII.



Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemuomba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuiunganisha Zanzibar na Arusha kwenye sekta ya utalii ili kuwezesha mabadilishano ya Watalii wa pande hizo mbili.


Aidha Makonda amemuomba Rais Mwinyi kutangaza fursa na vivutio vya Uwekezaji vilivyopo Mkoani Arusha katika adhma ya kutimiza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuongeza vyumba na Vitanda vya kulala wageni mkoani hapo.



Makonda ametoa maombi hayo leo Mei 17, 2024 wakati Rais Mwinyi akifungua semina ya uwekezaji na elimu ya fedha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanahisa wake na Watanzania kuelekea Mkutano Mkuu wa 29 wa Wanahisa utakaofanyika Jumamosi Mei 18, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).



Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa huyo ameishukuru benki ya CRDB kwa kuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya Mkoa wa Arusha pamoja na kuuchagua mkoa huo  kuwa mwenyeji wa semina na mikutano yao mikuu suala linalowanufaisha wafanyabiashara na wananchi mbalimbali wa mkoa huu,.



Katika majibu yake Rais Dkt.  Mwinyi amemuahidi Makonda kuwa atatekeleza maombi yake ipasavyo hasa katika suala la uwekezaji wa ujenzi wa hoteli na nyumba za kulala wageni kutokana na idadi kubwa ya Wawekezaji wanaofika Zanzibar kutaka kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba na vyumba vya kulala wageni na watalii wanaofika nchini.


Akiapishwa mwishoni mwa mwezi Machi Mwaka huu na Rais wa Samia alimuagiza Makonda kukuza utalii wa Arusha pamoja na kuongeza idadi ya vyumba na vitanda vya kulala wageni na watalii kutokana na upungufu mkubwa unaotokana na matokeo chanya ya filamu ya 'The Royal Tour Tanzania' iliyokuwa na nia ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania ikiwemo vile vilivyopo mkoani hapa kilipo kitovu cha Utalii Kaskazini mwa Tanzania.



Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay alisema benki hiyo ikiwa benki ya kizalendo inayomilikiwa na Watanzania kwa zaidi ya asilimia 80, inajivunia kuendelea kukuza thamani ya uwekezaji wa wanahisa wake ikiwamo Serikali ambayo inamiliki asilimia 36 ya hisa katika benki hiyo.


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni mwanahisa wa Benki hiyo kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar (ZSSF). Dkt. Laay amewakaribisha Watanzania wengine kuwekeza ndani ya Benki ya CRDB ili nawao waanze kunufaika na gawio nono ambalo limekuwa likitolewa na Benki hiyo.



Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela alisema malengo ya semina hiyo ni kuwajengea uwezo Wanahisa wao pamoja na Watanzania wengine ili kuwajengea uwajibikaji wa kifedha na kuongeza ushiriki katika fursa za uwekezaji hususan katika soko la hisa la Da es Salaam.


Kwa kutoa elimu hii Wanahisa wetu pia wanapata kufahamu zaidi faida za kuwekeza katika Benki yao ya CRDB, hivyo basi kuongeza uwekezaji na kupata faida nono zaidi, lakini pia kuwahamasisha na Watanzania wengine pia kuwekeza katika hisa hususan za Benki ya CRDB na kuanza kupata gawio,” aliongezea Nsekela.


Aidha, Nsekela alimshukuru Rais Mwinyi kwa ushirikiano wa kimkakati na mazingira mazuri ya biashara ambayo ndio chachu ya utendaji mzuri wa benki hiyo. Kadhalika, alimhakikishia Mheshimiwa Rais kuwa Benki ya CRDB  itaendelea kuwezesha uchumi wa Zanzibar kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo hususan katika kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa za Uchumi wa Buluu.


Katika semina hiyo, mada mbalimbali zilijadiliwa, ikiwa ni pamoja na Ujumuishi wa Kifedha, Uwekezaji katika Hisa, Hatifungani ya Kijani ya Benki ya CRDB, Wosia na Mirathi, pamoja na Kinga dhidi ya Majanga

"Yanga Yatawazwa Mabingwa wa Ligi Kuu NBC Premier League Baada ya Ushindi Dhidi ya Mtibwa Sugar"


Na Said Humbe





Klabu ya soka ya yanga imetawazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu soka NBC PREMIER LEAGUE baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 1-3 dhidi ya mtibwa sugar katika dimba la Manungu Turiani mkoani Morogoro.


Baada ya ushindi huo yanga wamefikisha point 71 ambazo haziwezo kufikiwa na klabu yeyote inayoshiriki ligi kuu msimu  huu wa 2023/2024 na kutawazwa kuwa mabingwa. 

Huku ukiwa ni ubingwa wao wa 30 tangu klabu hiyo ianzishwe katika ligi kuu mwaka 1936 magoli ya yanga yalifungwa na Kennedy Musonda, Clement Mzize pamoja na goli la kujifunga la Nasri Kombo huku goli la Mtibwa likifungwa na Charles Ilanfya .