ANAPA ILIVYOBADILI MAISHA YA WANAUMANGU


UMOJA wa Maendeleo ya Wanawake Ngurdoto,(UMANGU), umeeleeza namna Hifadhi ya Arusha, (ANAPA) iivyoweza kubadili  maisha yao kiuchumi baada ya kuwawezesha kufanya biashara ya ufugaji wa nyuki ambapo kwa sasa wanauza  asali yao nchini Italia.

Aidha wamesema ANAPA imewaletea wafadhili ambao wamewapa elimu ya ujasiriamali  ambapo mbali ya kuuza asali lakini wanatumia mazao mengine ya enyuki kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo  mafuta ya kujipaka.

Wameyasema hayo hivi karibuni wakati wakizungumza na Raia Mwema ilipowatembelea ofisi zao walizojenga kwenye kijiji Cha Ngurdoto kata ya Maji ya Chai wilayani Ngurdoto.



Katibu wa kikundi hicho Sarah  Mwakiabala amesema kuwa mbali ya kuwapa mizinga kwa ajili ya ufugaji wa nyuki lakini pia waliwaungalisha na wadau mbalimbali kwa ajili ya kuwapa elimu sanjaro na kuwaunganisha na masoko ya kuuza bidhaa zao.

"ANAPA walituunganisha na Hatari Lodge iliyopo ndani ya hifadhi hiyo ambao wanatufadhili na ndiyo wateja wetu wa kubwa wa mboga tunazolima kioganiki kwani hatutumii mbolea wala viatilifu vya viwandani.Tunatumia mbolea ya ya mboji," amesema Sarah .


Amesema kuwa Hatari Lodge wamekuwa wakipeleka watalii  wanaofika kwenye hoteli yao ili wajifunze utamaduni wao  kwa kuangali shughuli za ujasiriamali na kilimo cha mboga  tunazofanya kama kikundi ambapo mbali ya kununua bidhaa pia hupendelea kula chakula cha asili wanachowapikia ambacho hukilipia hivyo kuzidi kutunisha mfuko wa kikundi.

"Tunawapa chai ya mchaichai kwa viazi vitamu, mihogo, magimbi, maboga na hufurahia vyakula hivyo ambavyo tunaviandaa wenywewe hapahapa," amesema Sarah.

 
Katibu huyo wa kikundi cha UMANGU amesema kuwa kikundi hicho kilianza mwaka 1994 wakiwa na  mizinga 14 ambapo ANAPA iliwaunga mkono kwa iuwapatia  mizinga 50 ya kufuga nyuki.

"Ilitunyanyua sana kwani tulikuwa hatujui tunapata wapi fedha za kupeleka watoto shule lakini tulipopata mizinga hiyo 50 mambo yalibadilika.Tumeweza kusomesha wetu," amesema Sarah na kuongeza.

...Baadaye walituongezea mizinga mingine 100 na mpaka sada hivi mkiona hatua kubwa kimaendeleo tuliyoipiga ni kutokana na ANAPA wametusaidia sana tumeondokana na umaskini,".

Mwanakikundi, Sarah Mtema amesema kuwa ANAPA wamekuwa majirani zao wema kwani mbali ya kuwawezesha kufuga nyuki lakini wamewasaidia kupata soko la asali yao nchini Itali na baadhi ya wanakikundi waliwahi kushiriki maonyesho ya bidhaa kwenye nchi hiyo iliyo barani Ulaya.


"Tunasafiri kwenye maonyesho mbalimbali hata hapa nchini hasa yale ya nanenane tunauza sana bidhaa zetu huko. Kuna wanawake walioenda Itali kwa ajili ya kuuza asali ya nyuki wadogo ila kwenye maonyesho mengine tunapeleka bidhaa tunazotengeneza kwa majani ya migomba na shanga,"anasema Mtema na kuongeza.

"...Badala ya umbea wakinamama tunalima tunazalisha mbogamboga kiogaiki tunafungasha mbegu zake tunauzs tunapata kipato cha kutunza familia zetu kwa sasa sisi so tegemezi tena ANAPA imetukomboa"

"Tulijiongeza tukaanzisha bustani za mboga na ANAPA walitujengea bwawa la samaki tukawa tunauza lakini kutokana na ukame kwa sasa bwawa limekauka,".

Mtema anasema kuwa asali yao ni nzuri sana kwa sababu kama ile ya nyuki ya nyuki wadogo ambayo mizinga wameifunga ambapo  kwenye maeneo yao ambapo kuna miti ya aina mbalimbali hivyo huwawezesha nyuki hao kupata maua ya aina tofautitofauti.


"Nyuki wakubwa ni wakali sana ndiyo sababu mizinga yao tunaweka pembezoni mwa mto na inasababisha nyuki wasiende kwenye mashamba yanayopigwa dawa hivyo asali zetu za nyuki wadogo na wakubwa zote hazina kemikali," alisisitiza Mtema.

Mwanakikundi mwingine, Frida Munisi ni mmoja ya wanakikundi wa UMANGU  waliofanikiwa kwenda kwenye maonyesho ya bidhaa nchini Italia.

" Hii asali ya nyuki wadogo ilinifanipa mafanikio nilipanda ndege kwa mara ya kwanza hivyo kikundi hiki kimenifanikisha sana," anasema Munisi ambaye ni mama wa umri wa makamo na kuongeza.

...Mpaka sasa Italia  ni wateja wetu wazuri hivyo tunawauzia asali hii ya nyuki ndogo na wamekuja wakatupeleka Nakuru nchini Kenya wakatufundisha kutengeneza bidhaa kutokana na mazao ya nyuki  ikiwemo dawa krimu na lotion propolis,".

Mweka hazina wa UMANGU, Esther Sule amesema kuwa unaweza kutofautisha asali ya nyuki wadogo na wakubwa kwa kuionja ambapo ile ya nyuki wadogo ni chachu huku ike ya nyuki wakubwa ikiwa tamu.

"Asali ya nyuki wadogo ni chachu kwa sababu wao hufuata maua mbali sana na wanachukua kwenye maua tofautitofauti ndiyo sababu n asali hii hutumika kama dawa wakati ile ya nyuki wakubwa ambayo ni tamu iitumika kama chakula huku ikijenga mwili na kuongeza joto mwilini," alifafanua .Sule.

Naye mwanakikundi, Odilia Malisa anasema kuwa alijiunga na UMANGU mwaka 2000 ambapo amepata manufaa makubwa kuwa kwenye kiundi hicho.


"Mimi nilikuwa mama wa nyumbani tu sikuwa na kitu cha kuniingizia kipato, ANAPA walitupa mizinga ya nyuki 50 na wakawa wanatupatia mafunzo jinsi ya kurina asali na namna bora ya kutundika mizinga  mimi sikuwa najua," alisema Malisa na kuongeza

...Mvua ilikuja kubwa ikaharibu ile mizinga lakini ANAPA hawakutuacha wakatupa mizinga mingine 100 lakini ikawa inajaa maji inaozakutokana na mvua  nyuki wanahama hivyo hatukupata sana faida lakini ANAPA hawakutuacha wakatuletea mizinga mingine 50 ndiyo hii tunayo mpaka sasa,".

"Walituletea mashirika mengi kutusaidia  kwa kweli wametusaidia mafunzo mbalimbali ya kusindika matunda na nimeweza kusomesha wajukuu zangu walikuwa hapo nyumbani sasa wamehitimu wananitumia fedha nafurahi sana,".
Baadhi ya wanakikundi wa UMANGU


"Hili jengo la shule ya chekechea  tumejenga kutokana na miradi yetu tunayoiendesha baada ya ANAPA kutuunganisha na watu waliotupa elimu ya usindikaji, ujasiriamali kwani tunatengeneza bidhaa mbalimbali kama sabuni, mafuta ya kupaka kwenye ngozi.".

ANAPA wamekuwa wakisaidia jamii zinazoishi maeneo kuzunguka hifadhi hiyo kupitia mradi wa ujirani mwema.





 







0 Comments:

Post a Comment